Keifo FM

152 wahitimu kitado cha sita,16 washindwa kutokana na utoro Kyela day

19 April 2024, 20:35

Pichani ni mkurugenzi wa kampuni Basai General Suplies Ltd Baraka Mwamengo ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mahafari ya kumi na mbili ya kidato cha sita Kyela Sekondari Picha na James Mwakyembe

Mdau wa maendeleo na mkurugenzi wa kampuni ya Basai General Suplies Ltd Baraka Mwamengo ametoa jumla ya shilingi milioni moja na kuahidi kuwapatia mashine nyingine mpya ya kisasa kwaajiri ya kuchapia mitihani shuleni hapo ili kuondokana na kadhia hiyo.

Na Nsangatii Mwakipesile

Mahafari ya kumi na mbili ya kuwaaga wanafunzi wa kidato cha sita katika shule ya sekondari Kyela day yamefanyika hapa wilayani kyela huku mgeni rasmi akiwa ni mdau wa maendeleo na mkurugenzi wa kampuni ya  Basai General Suplies Ltd Baraka Mwamengo ambapo ametoa jumla shilingi milioni pamoja na kuahidi namna ya kupata mashine nyingine.

Akizungumza katika kilele hicho cha kuwaaga wanafunzi hao Mwamengo ameupongeza uongozi wa shule ya sekondari ya Kyela kwa namna ambavyo wamefanikiwa kuwatunza watoto hao hata kufikia hatua ya kuhitimu katika elimu yao ya sekondari,

Sauti ya Mwamengo akizungumza kuhusu pongezi kwa uongozi wa shule.

Pia Mwamengo amempongeza raisi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hasan kwa kuwezesha watoto wa kitanzania hususani wahitimu hao kwa mpango wake wa kuwezesha elimu bila ada pamoja na kuwataka wanafunzi hao kuenda kuwa alama nzuri katika jamii inayowazunguka.

Sauti ya Baraka Mwamengo akizungumza kuhusu pongezi zake kwa raisi SAMIA.
Pichani ni wanafuzni wahitimu wa kidato cha sita shule ya sekondari kyela day wakiwa katika picha ya pamoja mbele ya mgeni rasmi Baraka Mwamengo

Katika hatua nyingine Mwamengo amewataka wanafunzi wengine wanaobaki shuleni hapo kusimama imara katika kuhakikisha wanazingatia masomo ili kuisimamisha sifa ya shule ya Kyela day pamoja kuwatka walimu kuendelea kusimamia miiko ya ualimu ili kuwa na taifa lililobora.

Akisoma risala mbele ya mgeni rasmi Wiliumu Alex Mhitimu wa kidato cha sita shule hapo amepongeza walimu kwa upendo wao ambapo amesema walianza jumla ya wanafunzi 168 mwaka 2022 ambapo jumla ya wanafunzi 152 ndio wamefanikiwa kuhitimu kotokana na sababu mbalimbali ikiwemo utoro.

Sauti ya wilium Alex mhitimu wa kidato cha sita akisoma risala mbele ya mgeni rasmi Baraka mwamengo

Akijibu risala hiyo Mwamengo ameahidi kulibeba suala zima la mashine pamoja na kuangalia namna ya kufanikisha upatikanaji wa viti vya kukalia ambavyo vimeonekana kuwa sehemu ya changamoto shuleni hapo huku akitoa jumla ya shilingi milioni moja keshi kama motisha kwa walimu shuleni hapo.

Sauti ya Baraka Mwamengo akijibu kuhusu changamoto zilizojitokeza kwenye risala.
Pichani mgeni rasmi Baraka Mwamengo akipokea risala kutoka kwa Wilium Alex mwanafunzi anayehitimu kidato cha sita kyela sekondari’

Mahafari hayo ni ya kumi na mbili shuleni hapo ambapo jumla ya wanafunzi 168 walianza safari ya masomo yao mwaka 2022 inayokoma mwaka huu wa 2024 ikiwa na wanafunzi 152 huku wengine wakitajwa kuhama na wengine kushindwa kuendelea na masomo yao kwa sababu za utoro.