Keifo FM

Mfungata:Tutaendelea kujenga lami zaidi Kyela

16 December 2023, 11:27

Picha ya Mhandisi wa TARURA wilaya ya Kyela Karim Mfungata.Picha James Mwakyembe

Serikali ya Tanzania chini ya Raisi Samia Suluhu Hasani imepanga kujenga barabara zinazogawa mitaa ndani ya Wilaya ya kyela katika bajeti ya 2023-2024.

Na Nsangatii Mwakipesile

Wakati serikali ikiendelea kutekeleza Miradi mbalimbali hapa nchini mhandisi wa TARURA Karim Mfungata ametoa shukrani kwa wananchi wilayani Kyela kwa ushirikiano wanaompa katika utekerezaji wa miundombinu iliyochini yake mijini na vijijini.

Hayo yamejiri mapema leo wakati akizungumza na Keifo Fm akiwa ofisi kwake ambapo Mfungata amesema tangu afike ndani ya wilaya ya Kyela hajawahi kukumbana na kadhia yoyote iliyopelekea kukwama kwa kazi zake tofauti na maeneo mengine.

Sauti ya Mhandisi Karimu Mfungata akiwashukuru wananchi

kuhusu ujenzi wa barabara zinazoendelea kujengwa kwa kiwango cha lami hapa wilayani kyela amesema TARURA wanaendelea na ujenzi maeneo mbalimbali hasa hapa mjini ambapo amebainisha kuwa barabara zote zinaendelea kujengwa zitajengwa kwa kiwango cha lami.

Sauti ya Mhandisi Karimu Mfugata akieleza juu ya utekelezaji wa barabara
Picha ya barabara ya Siasa Road ikiwa katika hatua za ujenzi picha na James Mwakyembe

Kuhusu mikakati iliyopo kwa mwaka ujao Mfungata amesema ni kuendeleza kuboresha matengenezo zaidi kama ujenzi wa matuta pamoja na kujenga barabara zingine kwa kiwango cha alami mjini na vijijini.

Sauti ya Mhandisi Karimu Mfugata akieleza juu ya bajeti ijayo

Aidha Mfungata amewataka wananchi kuitunza miuondombinu ya barabara zote zilizokwisha kujengwa na kumshukuru raisi wa jamahuri ya muungano wa Tanzania kwa kutoa fedha nyingi zinazoendelea kuwaletea tija wakaazi wa kyela.

Sauti ya Mhandisi Karimu Mfugata shukrani kwa raisi na mbunge

Kukamilika kwa baadhi ya barabara kwa kiwango cha lami ndani ya wilaya ya Kyela kunatazamiwa kupunguza kadhia kubwa ya maji kujaa katika makazi ya watu kutokana na jiografia ya wilaya kukumbwa na mafuriko yanayotokana na mvua nyingi zinazopatikana katika majira ya mwaka.