Keifo FM

Kinanasi: Yajayo Kyela yanafurahisha

14 September 2023, 19:21

Picha ya mbunge wa jimbo la Kyela Ally Mlagila Jumbe Kinanasi na wananchi wa kata ya Bujonde akizindua daraja lililojengwa na wananchi . Picha na Benard Mwakipesile
This image has an empty alt attribute; its file name is img-20230914-wa0008-461x1024.jpg

Mbunge wa Jimbo la Kyela Ally Mlagila Jumbe Kinanasi ameahidi kutekeleza mambo yote yaliyoombwa na wananchi wa kata ya Bujonde ikiwemo barabara ya kutoka Bujonde kwenda Nyerere ndani ya kata hiyo. 

Ameyasema hayo wakati wa ziara yake ya kikazi katika kata hiyo huku akiwaasa wananchi kuongeza ushirikiano kwa ajili ya maendeleo binafsi na taifa kwa ujumla.

Sauti ya mbunge Ally Mlagila Kinanasi akihimiza ushirikiano

             

Aidha Kinanasi amewatoa hofu wananchi wa kata hiyo juu ya suala la bei ya kokoa  kwani ni adha iliyowakumba kwa muda mrefu.

Sauti ya mbunge akihimiza zao la kokoa

            

Katika hatua nyingine Kinanasi amewapongeza wananchi wa jimbo la Kyela  kwa kuwa na umoja licha ya utofauti wa kivyama  na tofauti nyinginezo.

Sauti ya mbunge akihimiza umoja

              

Aidha mbunge Kinanasi amewashukuru wananchi kwa kujitokeza katika ziara hiyo ambayo ilihusisha uzinduzi wa  madaraja mawili ya kata hiyo yaliyojengwa na wananchi wa kata ya Bujonde.