Keifo FM
Keifo FM
3 March 2026, 2:39 pm

“Kwenye jambo hili huu ni mwarobaini wa uchafuzi wa mazingira, tutakomesha kabisa upatikanaji wa taka ngumu katika mji wetu wa Kyela”.
Na James Mwakyembe
Ili kukabiliana na kadhia ya uchafu wa mazingira ya mji wa Kyela mtambo wa kubana na kufunga taka ngumu umefungwa na kuanza kazi rasmi katika kata ya Mbugani wilayani Kyela.
Mtambo huo wenye uwezo wa kubana na kufunga taka ngumu kiasi cha tani moja kwa siku umefungwa katika kitongoji cha Butiama jambo linaloleta mwanga mpya wa kupunguza wimbi la uchafu wa mazingira ya kitongoji na kata kwa ujumla.

Akizungumza na Mwandishi wetu mmiliki wa mtambo huo Abdalah Abdulahiman amesema lengo la kufunga mtambo huo ni kufungua fursa ya ajira kwa vijana hapa wilayani sambamba na kukabiliana na suala zima la uchafuzi wa mazingira.

Kupata undani wa habari hii tunaungana na mwandishi wetu James Mwakaligemo ambaye muda mfupi uliopita amezungumza na mmiliki huyo.