Keifo FM
Keifo FM
9 June 2026, 2:20 am

“Kilichonileta kwenu ni upendo tuu wanalusungo,nimekuja ili tulie pamoja na tuhuzunike pamoja”.
Na James Mwakyembe
Baada ya kadhia ya mafuriko yaliyoikumba kata ya Lusungo miezi miwili iliyopita diwani wa viti maalumu chama cha mapinduzi na mlezi wa kata ya Lusungo kupitia jumuiya ya wanawake wilaya ya Kyela Anna Mosses Mwamakula ametoa mkono wa pole kwa wananchi wa kata hiyo ikiwa ni sehemu ya kuungana nao katika janga hilo.
Akitoa pole hiyo ya mahindi,chumvi na sabuni mbele ya wananchi waliojitokeza Mwamakula amesema amesukumwa kutoa kidogo hicho kama sehemu ya pole yake kutokana na kadhia zilizowakumba pamoja na kumshukuru diwani wa kata hiyo kwa namna alivyoshirikiana naye kufanikisha jambo hilo.

Wakitoa neno la shukrani mbele ya diwani huyo baada ya kupokea chakula hicho wananchi hao wamemuomba kuwapelekea kilio chao kwa serikali ya halmashauri ya wilaya ya Kyela juu ya kuwajengea kuta zilizobomolewa na mto Lufilyo na maji kuingia katika makazi yao na kusababisha nyumba kubomoka.
Pia wakaiomba serikali kupitia diwani huyo kuiagiza idara ya mazingira hapa halmashauri ya wilaya Kyela kutoa kibari cha kuwawinda na kuwavuna wanyama aina ya boka wanaotoka mto Lufilyo wanaovamia na kuharibu mazao yao hasa mpunga hali inayotishia kukosa chakula katika msimu huu wa mavuno.
Sauti ya wananchi kuhusu boko 33
Naye diwani wa kata hiyo Albert Mwaitenda amemshukuru diwani Anna Mosses Mwamakula kwa msaada huo wa chakula alioutoa kwa wanalusungo huku akiomba serikali na Ofisi ya mbunge jimbo la kyela kuona namna nyingine ya kuwafikia wananchi wake ili kuwanusuru na kadhia hiyo ya mafuriko pamoja na kuishauri serikali kuwafukuza boko katika makazi ya watu.

Msaada uliotolewa kwa wananchi wa kata ya Lusungo ni Mahindi debe kumi na sita,sabuni katoni mbili na chumvi kwa kaya kumi na sita zilizofika katika eneo hilo wakiongozwa na diwani mwenyeji wa kata hiyo na afisa mtendaji wake.