Keifo FM

Kyela:Mwakyambile atingisha zawadi ubingwa bodaboda polisi jamii amani cup 2026.

29 April 2026, 11:34 am

Mdau wa maendeleo na mkurugenzi wa kiwanda cha mafuta cha Covenant Edible Oil kilichopo Kikusya wilayani kyela Babylon Mwakyambile akikabidhi jezi kwa Afande OCD wilaya ya Kyela,tukio lililofanyika katika viwanja vya kituo cha Polisi wilaya ya Kyela,Na James Mwakyembe

Mkurugenzi wa kiwanda cha Covenanta Edible Oil Babylon Mwakyambile amekonga mioyo wa wapenda michezo wilayani kyela baada ya kumwaga tuzo za mshindi wa nne, mfungaji bora,golikipa bora,refa bora,kibendera bora,kikundi bora cha ushangiriaji na timu yenye nidhamu Polisi jamii amani cup 2026.

Na James Mwakyembe

Jumla ya shilingi milioni sita zimetolewa na mdau wa maendeleo wilayani kyela ambaye pia ni mkurugenzi wa kiwanda cha Covenant Edible Oil Babylon Mwakyambile ikiwa ni udhamini wa mashindano ya Bodaboda Polisi jamii amani cup 2026 yaliyohitimishwa jana katika viwanja vya Kipija Arena.
Mwakyambile ametoa udhamini huo kuanzia hatua ya timu kumi na sita kwa kutoa jezi seti moja kwa timu zote zilizoingia katika hatua hiyo ya kumi na sita bora michuano ya Bodaboda polisi jamii amani cup 2026 yakihusisha timu kutoka katika kata zote 33 zinazounda halmashauri ya wilaya ya kyela.
Akizungumza muda mfupi baada ya kuhitimishwa kwa mashindano hayo mwakilishi wa mkurugenzi wa kiwanda cha kuzalisha mafuta Covenant Edible Oil Frank Mwakapala amelishukuru jeshi la polisi wilayani kyela kwa kutambua umuhimu wao na kuwaomba udhamini wa mashindano hayo huku akitoa ufafanuzi wa jinsi zawadi zilivyotolewa.

Sauti ya frank mwakapala
Pichani ni miongoni mwa zawadi zilizotolewa kwa mgeni rasmi wa mashindano Mkuu wa wilaya Josephine Manase pamoja na wageni maalumu kutoka jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya na makao makuu Dodoma.

Akihitimisha Mashindano hayo mgeni rasmi mkuu wa wilaya ya Kyela Josephine Manase amewapongeza jeshi la polisi kuandaa mashindano hayo pamoja na kuwashukuru wadhamini wakuu mbunge wa jimbo la kyela Baraka Mwamengo na mkurugenzi wa kiwanda cha kuzalisha mafuta Covenant Edible Oil Babylon Mwakyambile.

Sauti ya mkuu wa wilaya ya kyela.

Mbali na kutoa udhamini huo pia Mwakyambile ametoa jezi seti moja na mpira kwa timu ya mpira wa miguu ya jeshi la polisi kyela,jezi zilizotumiwa kwa mara ya kwanza jana wakati timu hiyo ilipomenyana na kikosi cha timu ya Covenant Eible Oil katika mchezo wa mapema kabla ya fainali uliotamatika kwa sare ya bila kufungana,huku bingwa wa michuano hiyo akiwa ni bodaboda kata ya Ipinda iliyejinyakulia Ng’ombe mkubwa.