Keifo FM

Kyela: Vijana 10 wa greengard wakabidhiwa sare Itunge

8 March 2024, 16:27

Picha,vijana wa ccm itunge wakikabidhiwa sale aina ya kombati Na Emmanuel Jotham

Vijana wa chama cha mapinduzi uvccm  kata ya itunge wilayani kyela wamekabidhiwa sale aina kombati kwa ajili ya mandalizi ya uchaguzi wa serikali za mitaa 2024-2025.

Na Emmanuel Jotham

Vijana kumi (10) wa Green Gard walio kwenda mafunzo kupitia chama cha mapinduzi kata ya Itunge wilayani Kyela wamekabidhiwa sale na Mdau wa maendeleo Bablon Mwakyambile ili kutoa hamasa kwa vijana hao ya kukitumikia chama chao.

Akikabidhi sale hizo kwa niaba ya Bablon Mwakyambile Frank Mwakapala amesema bablon ameamua kutoa sale za GreenGard kwa vijana hao kumi wa Greengard ikiwa ni maandalizi mema ya kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa.

Mwakapala amesema Bablon yeye ni mwanachama wa chama cha mapinduzi na amameamu kufanya hivyo baada ya kupelekewa maombi na vijana hao kupatiwa sale ili kujiweka imara na uchaguzi wa serikali za mitaa kwa mwaka 2024-2025

Sauti ya mwakapala akikabidhi sale kwa vijana i

Aidha kwa upande wake mwenyekiti wa vijana chama cha mapinduzi kata ya itunge Yonah Mwakalinga amemshukuru mdau wa maendeleo Bablon Mwakyambile kwa kukubali ombi lao na kulitekeleza kitu ambacho amesema kimeleta hamasa kubwa vijana hao ndani ya chama cha mapinduzi.

Sauti ya mwenyekiti wakishukuru baada ya kukabidhiwa sale