Keifo FM

Strobeli yawageuza lulu wakulima wilayani Rungwe

29 November 2023, 22:53

Baadhi ya wakulima wa zao la strobeli wilayani Rungwe.Picha na James Mwakyembe

Tathmini ya kuangazia mafanikio ya zao la Strobeli wilayani Rungwe yamefanyika yakiongozwa na msemaji wa shirika lisilo la kiserikali Shoma Nangale.Na Nsangatii Mwakipesile

Baada ya kutambulishwa rasmi kwa zao la Strobeli wananchi wilayani Rungwe mkoani Mbeya wamelishukuru shirika la Kibo ardhi kwa kuwa chanzo cha mafanikio ya kuinua uchumi wa familia na serikali kwa ujumla.

Hayo yamejiri wakati wa tathmini ya miaka mitatu ya shirika lisilokuwa la Kiserikali la Eliventansi tangu kutambulishwa kwa zao hilo wilayani Rungwe.

Wamesema mpaka sasa wamepata manufaa makubwa kiuchumi kutokana na uzarishaji wa zao la strobeli ambao umewachukua muda mfupi ikilinganishwa na mazao mengine kama mahindi na ndizi.

wakulima wa zao trobeli wilayani Rungwe

Mmoja wa wanufaika wa zao Jotham Mwamalema amelipongeza shirika hilo binafsi la Eliventansi kwa kuwaletea kilimo hicho kwani kwa sasa yeye ni mnufaika namba moja na kukiri kuwa zao hilo limemuinua kiuchumi tofauti na hapo awali.

sauti ya jotham mwamalema

Akizungumza akiwa katika mashamba ya Vanila yaliopo Kitongoji cha Syukula wilayani Rungwe Shoma Nangale msemaji wa shirika lisilo la kiserikali la Elivetansi amesema mafanikio ni makubwa kwani mradi huo tangu uanziswe ni miaka mitatu mpaka sasa.

sauti ya Shoma Nangale mesemaji wa elevensi
Picha ya wakulima wa zao la strobelina viongozi

Shirika la Elivetasi ni shirika lisilo la kiserikali ambalo limekuwa nikijihusisha na masuala mbalimbali ya kijamii ikiwemo kilimo na Afya.