Keifo FM

Mwangungulu:Wazazi wapelekeni watoto wenye ulemavu shuleni 2024

11 December 2023, 16:17

Pichani ni Afisa Elimu elimu Maalum Wilaya ya Kyela Mwalimu Kanzale Mwagungulu.Picha na Masoud Maulid

Wakati dirisha la uandikishwa kwa watoto walio na umri wa kuanza shule kwa darasa la kwanza likifunguliwa jamii wilayani kyela imetakiwa kuwapeleka watoto wao kujiandisha ili kutimiza haki yao ya msingi ya kupata elimu.

Na Masoud Maulid

Wito umetoletewa kwa Wazazi na walezi wenye watoto wenye umri wa   kuanza  darasa la awali na darasa la kwanza kwa mwaka 2024 kuwaandikisha wakiwemo watoto wenye ulemavu.

Hayo yamezungumzwa na Afisa Elimu elimu Maalum Wilaya ya Kyela Mwalimu Kanzale Mwagungulu wakati akizungumza na mwandishi wa habari ambapo amesema   mzazi bila kujali ana mtoto mwenye ulemavu au asiyekuwa na ulemavu  amwandikishe kuanza masomo kwa mwaka 2024 kwakuwa elimu ni haki ya kila mtoto.

sauti ya Mwalimu Kanzale Mwagungulu kuhusu wazazi kupeleka watoto shule

Kanzale ameongeza kuwa serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania imeweka mikakati madhubuti kuhakikisha kila mtoto anapata elimu akiwemo mtoto mwenye ulemavu hivyo amesisitiza watoto hao wapelekwe kuandikishwa ili kupata haki yake ya elimu.

Katika hatua nyingine Kanzele amewatoa wasiswasi wazazi na walezi wa watoto wenye aina mbalimbali za ulemavu kwamba katika shule zilizopo halmashauri ya wilaya kyela zinauwezo wa kupokea watoto wenye ulemavu huku kwa watoto wenye ulemavu mkubwa wakitengewa  vituo maalumu.

Sauti ya Mwalimu Kanzale Mwagungulu kuhusu vituo vilivyongwa kufundisha watoto wenye ulemavu

Kutokana na baadhi ya wazazi na walezi kutompa nafasi ya kupata elimu mtoto mwenye ulemavu kwa kumficha na wengine kuona ni sehemu ya laana afisa huyo wa elimu amewathibitishia wazazi kwamba watoto wenye ulemavu wanauwezo wa kufanya mambo makubwa sawa na watoto wasiokuwa na ulemavu.

Sauti yaMwalimu Kanzale Mwagungulu kuhuusu kubainisha vituo

Zoezi la uandikishaji kwa wanafunzi wa awali na darasa la kwanza kwa mwaka 2024 tayari umeanza na mwisho wa uandikishaji kwa wanafunzi ni desemba 30 mwaka huku huku hatua kali zikichukuliwa kwa mzazi yeyote atakayepuuza agizo hilo