Keifo FM

Kisa Simba, Yanga bodaboda Kyela wasogeza mbele uchaguzi

30 November 2023, 22:27

Ofisi ya Umoja wa Bodaboda wilayani Kyela.

Uchaguzi wa kuwapata viongozi wa umoja wa bodaboda Kyela uliopangwa kufanyika Disemba 2, 2023 umesogezwa mbele mpaka Disemba 8, 2023.

Na Nsangatii Mwakipesile

Mwenyekiti wa uchaguzi wa waendesha bodaboda wilayani Kyela Widrey Mwasyeka ametangaza kusogezwa mbele uchaguzi wa chama hicho mpaka tarehe nane ya mwezi wa kumi na mbili mwaka huu wa 2023.

Awali uchaguzi huo ulipangwa kufanyika tarehe 2/12/2023 baadaya ya ule wa awali wa 24 octoba kuvunjika kutokana na wapigakura kutoridhika na mwenendo mzima wa uchaguzi huo.

Akitoa taarifa juu ya mabadiliko hayo Mwasyeka amesema sababu kubwa za kusogeza mbele uchaguzi ni pamoja na michezo inayohusisha timu kubwa mbili za Tanzania za Simba na Yanga kuwa uwanjani siku hiyo jambo ambalo lingewafanya kuwanyima uhuru wapigakura wao na sababu zingine ni suala la usalama.

Sauti Widrey Mwasyeka akizungumzia kuhusu uchaguzi kusogezwa mbele
Picha ya Widrey Mwasyeka Mwenyekiti uchaguzi wa bodaboda Kyela