Keifo FM

Swebe: Nipo tayari, CHADEMA nitume popote nitakwenda

8 January 2024, 16:02

Pichani ni wanachama wa CHADEMA wilaya ya Kyela wakiwa katika ukumbi wa kanisa la Kiinjri Moraviani Bondeni Kyela wakijiaandaa na zoezi la upigaji kura kuchagua viongozi mbalimbali Picha na Nsangatii Mwakipesile

Baada ya kushinda kwa kishindo katika uchaguzi wa ndani wa chama cha demokrasia na amaendeleo wilaya ya Kyela mwenyekiti mpya wa chama hicho Victoria Swebe amesema yuko tayari kukipigania chama hicho ili kitwae jimbo katika uchaguzi ujao.

Na James Mwakyembe

Uchaguzi wa ndani wa chama cha Demokrasia na Mendeleo Chadema kwa wilaya kyela umefanyika huku ikishuhudiwa mwanamama victoria Swebe akinyakua nafasi ya uenyekiti wa wilaya ya Kyela.

Swebe anachukua nafasi hiyo akiwashinda washindani wake watatu akiwemo mwenyekiti aliyekuwa akiishikiria nafasi hiyo kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita kwa zaidi ya kura 20 zilizopigwa na wajumbe wa chama hicho kikuu cha upinzani hapa nchini Tanzania.

Akizungumza mara baada ya kukamilika kwa zoezi hilo la uchaguzi ulifanyika katika kanisa la Kiinjiri Moraviani hapa wilayani Kyela msimamizi wa uchaguzi huo ambaye pia ni katibu mkuu wa chadema mkaoa wa mbeya Hamadi Mbeale amewapongeza wanachama wa CHADEMA wilaya ya Kyela kwa namna walivyojitokeza pamoja na kuwataka waliochaguli kuenda kufanya kazi iliyombele yao.

Sauti ya msimamizi wa uchaguzi Hamadi Mbeale akizungumza mara baada ta zoezi la uchaguzi kukamilika

Akitoa neno la shukrani baada ya kuchaguliwa kuwa mwenyekiti wa chama wilaya ya Kyela mwenyekiti mpya wa Chadema wilaya Victoria Swebe amewashukuru sana wajumbe walimchagua kwa nafasi hiyo huku akiwataka wanachadema wote wilaya ya Kyela kushikamana ili kujihakikishia katika uchaguzi ujao

Sauti ya mwenyekiti mpya CHADEMA wilaya ya Kyela Victoria Swebe akizungumza baada ya kuchaguliwa na wajumbe
Picha ya mwenyekiti mpya CHADEMA wilaya ya Kyela Victoria Swebe baada ya kuchaguliwa na wajumbe

Kwa upande wake Donald Mwaisango aliyechaguliwa na kutetea nafasi yake ya katibu mwenezi wa chadema wilaya yeye pia amewashukuru wapiga kura wote kwa kumuamini kwa mara nyingine tena licha ya kukiri kuwa ucgauzi huo kwa mara ya umekuwa mgumu taofauti miaka mingine

Sauti ya mshindi wa nafasi ya katibu mwenezi wa CHADEMA wilaya ya Kyela Donald Mwaisango

Akizungumza kwa niaba ya wapiga kura waliojikeza mfungwa wa kisiasa ambaye kwa sasa yuko huru baada ya kushinda rufaa yake Gerald Mwakitalu amekiri kuwa uchaguzi huo ulikuwa wa huru na haki hivyo kuwapongeza wote waliochaguliwa na kuwatakia kila lahri katika kukijenga chama kipya chenye nguvu zaidi.

Mmoja wa wajumbe aliyepata nafasi ya kuzungumza na keifo fm baada ya kumalizika uchaguzi huo Gerald Mwakitalu

Kufanyika kwa uchaguzi wa ndani kwa nagzi ya wilaya ya Kyela kunahitimisha rasmi michakato yote ya uchaguzi wa chama hicho ulioanza tangu mwaka jana wa 2023 ambapo viongozi mbalimbali wamechaguliwa katika kukiongoza chama hicho kwa kipindi kingine cha miaka mitano ijayo.