Keifo FM

Kyela:Barabara 21 zakarabatiwa Butihama

9 December 2023, 13:34

Pichani ni Mwenyekiti wa kitongoji cha Butihama hapa wilayani Kyela Yohana Mwambungu akiwa katika moja ya makaravati mapya yaliyojengwa.Picha na James Mwakyembe.

Wananchi wa kitongoji cha Butihama wameipongeza serikali kwa kufanikisha ujenzi wa barabara 21 pamoja na makaravati 14 hali iliyopelekea kutatua kadhia ya miundombinu chakavu kitonjojini humo.

Na Nsangatii Mwakipesile.

Wakati Tanzania ikiadhimisha miaka 62 ya uhuru wananchi wa kitongo cha Butiama hapa wilayani Kyela wameishuru serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania kwa kazi za kuwaletea maendeleo kitongojini humo.

Wakizungumza na mwandishi wa habari wananchi hao wamesema serikali kupitia mwenyekiti wao Yohana Mwambungu imeweza kufanikisha ujenzi na ukarabati wa miundombunu mbalimbali ya kijamii kitongojini humo hali ambayo imewafanya waishi kwa furaha na amani.

Wamesema miongoni mwa miundombinu iliyokarabatiwa ni pamoja na barabara kuu na zinazogawa mitaa zaidi ya ishiri pamoja na ujenzi wa makaravati mapya ambayo yametatua kadhia kubwa ya watoto na wanafunzi kushindwa kufika shule kwa wakati kutokana na maji kujaa miferejini.

Sauti ya wananchi wa Butihama wakishukuru

Akipokea pongezi hizo kwa niaba ya serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania Mwenyekiti Yohana Mwambungu ameshukuru serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hasan kupitia watendaji wake wanaomuwakilisha hapa wilayani kwani kama si umakini na uaminifu wao.

Pamoja na hayo Mwambungu amezitaja barabara zilizokwisha kukakarabitiwa pamoja na makaravati ndani ya kitongoji hicho,ambapo pia amewaomba wananchi wake kuwa walinzi wa miundombinu hiyo ili iweze kutumika kwa kipindi kirefu.

Sauti ya Mwenyekiti Yohana Mwambungu akishukuru Rais wa jamahuri ya muungano wa Tanzania.

Mwambungu  amehitimisha kwa kuwashukuru viongozi wa iwlaya ya Kyela wakiongozwa na Mkuu wa wilaya Bi Josephine Manase kwakuwa bega kwa bega katika maendeleo ya kitongoji hicho.