Keifo FM

Kyela:”Tunaogopa kuingia mtoni kisa mamba”

11 December 2023, 16:29

Pichani ni mto Mbaka unaohofiwa kuwa na Mamba wanaosababisha vifo kwa wananchi wanaozunguka mto huo ndani ya Kyela.Picha na Nsangatii Mwakipesile

Baadhi ya wananchi wanaouzunguka mto mbaka hapa wilayani Kyela wameiomba serikali ya halmashauri ya wilaya kyela kuwavuna mamba wanaongezeka kwa kasi katika mto mbaka.

Nsangatii Mwakipesile

Kufuatia ongozeko la wanyama aina ya mamba ndani yam to mbaka hapa wilayani Kyela zaidi ya watu wanne   wameuawa na mamba ndani ya mto mbaka katika kipindi cha miezi sita iliyopita.

Wakizungumza na mwandishi wa habari wahanga wa matukio hayo ambao ni wananchi wa kata ya Ipande wamesema kuwepo kwa ongezeko la mambo katika mto huo kumesababisha watu wane kufa kwa kuuawa na mamba hali inayowapelekea kuiomba serikali kulitatua jambo ambalo limewafanya kuishi kwa hofu.

Wamesema mpaka sasa hofu imetanda mioyoni mwao na kukosa uhuru wa kuutumia mto huo ambao wamekuwa wakiutegemea kwa shughuli za kiuchumi na nyumbani kutokana na kuhofia kuliwa na wanyama hao hatari.

Sauti ya wananchi wa mbula wanaozunguka mto mbaka miongoni mwa waliopoteza ndugu

Kwa upande wa mwemyekiti wa kijiji cha Mbula Alfred Mwalukuta amesema wanyama hao wamekuwa tishio na wanaogopa hata kuingia mtoni na kuiomba serikali kuwavuna mamba hao.

sauti ya Alfred Mwalukuta mwenyekiti akiomba serikali kuwavuna mamba mto mbaka

Stivini Mwangalaba diwani wa kata ya Ipande amekiri kutokea kwa vifo hivyo kutokana na wananchi wengi kuutumia mto huo kwa shughuli za kiuchumi na matumizi mbalimbali ya nyumbani.

Mwangalaba amesema tayari ameandika barua kwenda wilayani ikiitaka serikali kuwavuna mamba hao ili kuwapunguza katika mto huo na mpaka sasa wanasubiri majibu ya mkurugenzi wa halmashauri ya Kyela.

Sauti ya diwani wa kata ya Ipande stivini Mwangalaba kuhusu mamba na kutatua kadhia hiyo

Mto mbaka ni miongoni mwa mito mikubwa minne inayopatikana ndani ya kyela unaotiririsha maji yake kutokea wilaya jirani ya Rungwe ambao umekuwa muhimu mno kwa watu wa kyela wanaouzunguka mto huo kwa shughuli za kiuchumi.