Keifo FM

Kikao cha kamati ya tathmini chanjo ya polio chafanyika wilayani Kyela

13 September 2023, 10:25

Mwenyekiti wa kamati ya tathmini mkuu wa wilaya ya Kyela Josephine Manase akiongoza kikao. Picha na afisa habari wilaya ya Kyela

Kamati ya tathmini ya ugonjwa wa polio imeketi na kujadili masuala mbalimbali ya maandalizi kuelekea zoezi la chanjo ya polio ikiwemo namna ya kuwafikia watoto hasa wenye umri chini ya miaka minane.

Na Secilia Mkini

Kikao cha mafunzo dhidi ya kampeni ya chanjo ya Polio kwa kamati ya Afya ya msingi ngazi ya jamii (PHC) chafanyika wilayani Kyela,

Akiongea katika kikao hicho Mwenyekiti wa Kikao hicho ambae ni Mkuu wa wilaya ya Kyela Mhe. Josephine Manase amewataka viongozi wa ngazi zote kwenye jamii, kushirikiana na kutoa elimu sahihi kwa jamii ambazo wanaziongoza.

Aidha amewataka viongozi hao kutoa elimu juu ya imani potofu dhidi ya chanjo ya Polio, ili kuwafanya wazazi wengi kuwachanja watoto wao na kutimiza malengo ya idadi ya watoto tunaotaka kuwafikia katika wilaya yetu.

Nae Mratibu wa chanjo ndugu Rosemary Tesha amesema chanjo ni kinga hivyo mtoto anaweza kuchanjwa zaidi ya mara nne.

Pamoja na hayo mratibu wa chanjo ametoa sababu muhimu za kumpa mtoto chanjo ikiwa ni pamoja na kusaidia kupunguza gharama za matibabu, kumkinga mtoto dhidi ya magonjwa, kupunguza ulemavu, vifo kwa mtoto na kupunguza magonjwa ya mlipuko katika jamii.