Keifo FM

Wananchi Kyela washauriwa kuachana na imani potofu zoezi la utoaji chanjo kwa watoto

21 September 2023, 13:27

Watoa huduma wakiwa tayari kwa ajili ya zoezi la kutoa chanjo ya polio nyumba kwa nyumba. Picha na Secilia Mkini

Wakati zoezi la utoaji chanjo kwa watoto chini ya umri wa miaka 8 likianza hii leo wazazi na walezi wilayani Kyela wameaswa kuachana na imani potofu, bali wanatakiwa kuamini chanjo inayotolewa na watoa huduma waliowekwa na serikali.

Na Secilia Mkini

Katika kuhakikisha  zoezi la chanjo ya polio linafanikiwa, wananchi wilayani Kyela wameaswa kutoa uishirikiano kwa serikali ili watoto waweze kupata chano hiyo.

Haya yamejiri wakati wa kampeni ya utoaji elimu kwa jamii kupitia watoa huduma ya afya kwa jamii ambao wamewaasa wananchi kuepukana na imani potofu juu ya chanjo hizo na badala yake kila mzazi mwenye mtoto ahakikishe kuwa mwanae anapata chanjo hiyo .

voxpop watoa huduma

               

Katika hatua nyingine wameeleza namna wanavyowafikia wanajamii ili kuwapatia elimu ikiwemo katika shughuli mbalimabali za kijamii kama sherehe na maafa.

Kwa upande wake katibu wa watoa huduma ya afya ngazi ya jamii Bakari Samson amewaasa wazazi na walezi kuhakikisha wanatoa ushirikiano kwa serikali ili kufikia malengo yaliyopangwa na serikali .

                           

Sauti ya katibu wa watoa huduma