Keifo FM

Convenant Edible Oil Ltd yamwaga vifaa vya michezo Kajunjumele Kyela

27 March 2024, 13:01

Pichani ni mwakirishi wa mkurungenzi wa kampuni ya Convenant Edible Oil Frank Mwakapala akiwa na viongozi wa chama cha Mapinduzi kataya Kajunjumele Picha na James Mwakyembe

Kampuni ya kuzarisha mafuta ya Kyela Cooking Oil Convenant Edible Oil Ltd chini mkurugenzi Babylon Mwakyambile wamekabidhi mipira nane kwa timu nane shiriki katika ligi ya chama cha Mapinduzi ccm kata ya Kajunjumele.

Na Nsangatii Mwakipesile

Mkurungenzi wa kampuni ya Convenant Edible Oil Ltd wazarishaji wa mafuta ya Kyela Cooking Oil Babylon Mwakyambile amakambizi Mipira Nane katika kata ya Kajunjumele yenye thamani ya zaidi ya shilingi laki nne hapa wilayani kyela.

Tukio hilo limefanyika mala baada ya kutamatika kwa mashindano ya chama cha mapinduzi [CCM] na kushawishi vijana kijisajiri katika mfumo wa kietroniki na kuchukua kadi ili kujenga afya kwa vijana ndani ya kata hiyo.

Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hioyo hivyo kaimu Mwakirishi wa mkurugenzi Frenk Mwakapala amewasihi vijana kujituma na kucheza kwa malengo kwani kwa sasa mpira ni ajira.

Pia amewatoa hofu kwamba kamuni hiyo iko tayari kushiriikiana nao wakati wowote panapohitajika vifaa vya michezo ili kukuza vipaji vya vijana wa kata hiyo.

Sauti ya mwakirishi wa mkurugenzi Frank Mwakapala akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo vya michezo.
Mwakirishi wa Mkurugenzi Kampuni ya Convernt Edible Oil Frank Mwakapala akikabidhi mpira kwa timu shiriki

Kwa upande wa katibu wa Umoja wa vijana kata ya Kajunjumele Richard Mwaipungu amemshukuru Babylon Mwakyambile kwa vifaa hivyo huku akikiri kuwa kwa moyo aliouonesha ni moyo wa kizalendo na upendo kwa tarifa ya mwaliko aikuchukua  muda mwingi hata kujibiwa maombi yao yaliyopelekea kupewa vifaa hivyo bora vya kimichezo vitakavyokuwa msaanda katika tasnia ya michezo kwao.

Sauti ya katibu wa Umoja wa Vijana Kata ya Kajunjumele  Richard Mwaipongo akimshukuru Babylon Mwakyambile kwa vifaa hivo vya mechezo.

Pia wawakirishi wa timu zilizo shiliki kwenye mashindano hayo ya ndani ya kata ya Kajunjumele wameshukuru mdau huyo na kuahidi kwenda kutengeneza timu zao na kishiriki mashindano makubwa zaidi ndani na nje ya kata hiyo.

Sauti ya wawakirishi wa Timu shiriki wakimshukuru Babylon Mwakyambile kwa Vifaa hivyo.
Pichani Mamia ya watazamaji waliojitokeza kuangalia mchezo wa fainali katitika viwanja vya shule ya sekondari kajunjumele kati ya kajunjumele sekondari vs Cossovo fc.

Timu zilizokabodhiwa mipira ni pamoja na,Mbeya City ya kajunjumele,Mbala Boy’s,Cossovo,Beach Boy’s,Soweto fc,Mapinduzi,New Boy’s,Mpanga fc.

Mashindano hayo yalianza tangu mwezi wa pili yakianza na timu kumi na nne ambapo timu nane zilizofanikiwa kusonga mbele kwa hatua ya robo fainali ndizo zimekabidhiwa mpira mmoja kwa kila timu.