Keifo FM

Kumekucha uchaguzi CHADEMA Kyela

30 November 2023, 22:13

Pichani ni Jengo la Ofisi ya Chama Chama Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Picha na Nsangatii Mwakipesile.

Hekaheka za kuwapata viongozi wa nafasi mbalimbali ndani ya chama cha Demokrasia na Maendeleo zimepamba moto hapa wilayani Kyela mkoani mbeya.

Na James Mwakyembe

Zoezi la uchukuaji fomu kugombea nafasi mbalimbali ndani ya chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA limeanza rasmi wilayani Kyela huku ikishuhudiwa Victoria Swebe akichukua fomu ya kugombea nafasi ya mwenyekiti wilaya ya Kyela.

Hayo yamejiri mapema leo katika ofisi za chama hicho hapa wilayani Kyela ambapo mtia nia huyo ametanabaisha sababu za yeye kuchukua uamuzi wa kuingia katika uchaguzi huo muhimu kabisa kwa wanachama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA.

Sauti ya Victoria Swebe mtia nia wa nafasi wa Uenyekiti wilaya Kyela
Picha ni Victoria Swebe

Kwa upende wake Deus Wilson Mwakilasa mgombea wa nafasi ya katibu mwenezi wa chama hicho wilayani Kyela yeye amemshukuru Donard mwaisango anayemaliza muda wake na kusema endapa atapata nafasi hiyo basi atahakikisha anaitendea vyema nafasi hiyo.

Sauti ya Deusi Mwakilasa akieleza sababu za kuchukua fomu ya uenezi wilaya

Ngamanya Simon mwakasula mgombea nafasi ya mjumbe wa mkutano mkuu taifa amewaomba wanachama wa CHADEMA hapa wilayani Kyela kumuamini na kumpa nafasi ya kuwatumikia katika nafasi hiyo muhimu kwa ustawi wa chama ili kukijenga chama imara.

sauti ya Ngamanya Mwakasula akieleza utayari wake kuwania nafasi ya ujumbe taifa

Uchanguzi wa ndani wa chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA umeanza katika maeneo mbalimbali hapa wilayani Kyela ikiendelea kushuhudiwa wanachama mbalimbali wakijitokeza kuchukua fomu za kugombea nafasi za uongozi katika chama hicho kikuu cha Upinzani hapa Nchini.