Keifo FM

Madereva 87 Kyela wakabidhiwa vyeti vya udereva

21 September 2023, 17:54

Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya ACP Benjamin Kuzaga akiwa katika picha ya pamoja na madereva waliokabidhiwa vyeti. Picha na James Mwakyembe

Na James Mwakyembe

Jumla ya madereva themanini na saba wapepigwa msasa wa mafunzo ya udereva na  kukabidhiwa vyeti vya udereva huku wakitakiwa kuwa mabalozi wazuri wawapo barabarani.

Madereva 87 waliokabidhiwa vyeti katika picha

Katika kuhakikisha ajali za barabarani zinapungua mkoani Mbeya, jeshi la polisi limetoa vyeti vya uhitimu kwa madereva themanini na saba hapa wilayani Kyela.

Akikabidhi vyeti hivyo kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya ACP Benjamini Kuzaga amewataka wahitimu hao wa mafunzo ya udereva kuhikisha wanayatumia vyema mafunzo hayo waliyoyapata ili kupunguza ajari.

Sauti ya kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya ACP Benjamini Kuzaya

ACP Kuzaga ameongeza kwa kuwataka wahitimu hao kuhakikisha wanatii sharia bila shuruti pamoja kufuata sheria zote za usalama  barabarani huku akisisitiza kuwa jeshi hilo litakuwa kali kwa madereva wote wenye kujirudia kwa matukio ya uzembe barabarani

Sauti ya kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya ACP Benjamini Kuzaya

Kwa upande wake mwaenyekiti wa kamati ya usalama barabarani Mkoa wa Mbeya amewataka wahitimu hao kuhakikisha wanakuwa mabarozi wazuri pamoja na kubainisha idadi ya wahitimu wa mafunzo hayo ya udereva kwa wilaya ya Kyela.

Sauti ya mwenyeki kamati ya usalama barabarani mkoa wa Mbeya

Wakizungumza kwa furaha baada ya kupokea vyeti vyao vya uhitimu wa mafunzo ya udereva hapa wilayani Kyela wamemshukuru ACP Kuzaga na chuo cha KPC kilichofanikisha wao kupata vyeti vyao na kuiomba serikali kutilia mkazo chuo hicho kupata wanafunzi wengi Zaidi ili kitambulike nchini kote.

Sauti ya madereva wahitimu Kyela 

Mafunzo ya udereva kwa madereva hapa wilayani Kyela yamehitimishwa kwa kukabidhi vyeti kwa jumla ya madereva themanini na saba ambao miongoni mwao ni madereva wa matraki,mitambo Abiria na Beziki.