Keifo FM

Mwangasa:Vijana shikamaneni acheni makundi

11 January 2024, 18:09

pichani ni mjumbe wa UWT mkoa wa Mbeya Sarah Mwangasa akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa wilaya Picha na James Mwakyembe

Katika kuiimarisha jumuiya ya vijana Uvccm hapa wilayani Kyela mjumbe wa mkutano mkuu mkoa wa mbeya Sarah Mwangasa amewataka vijana wilayani hapa kuachana makundi ili kukijenga jumuiya imara.

Na Nsangatii Mwakipesile

Mjumbe wa UWT mkoa kutoka wilayani Kyela Sarah Mwangasa ametoa projecta yenye thamani ya shilingi milioni moja na laki tano kwa jumuiya ya vijana ya chama cha mapinduzi CCM wilaya ya kyela.

Mwangasa ametoa kifaa hicho baada ya kuwepo changamoto ya vifaa vya kuendeshea mafunzo kwa jumuiya hali iliyolazimu mjumbe huyo wa mkoa wa mbeya kuguswa na kuchangia projecta hiyo.

Akikabidhi Projecta hiyo kwa katibu wa jumuiya ya vijana wilaya ya Kyela Mwangasa amewapongeza vijana wilayani kyela kwa kuweka utaratibu wa kuwa na mafunzo hali aliyoitaja kuwa itasaidia katika kuikuza jumuiya hiyo muhimu kwa chama cha Mapinduzi.

Sauti ya mjumbe wa mkutano mkuu UWT mkoa wa Mbeya Sarah Mwangasa
Pichani ni Sarah Mwangasa akimkabidhi projecta ya kisasa katibu wa jumuiya ya vijana wilaya ya kyela.

Katika hatua nyingine Sarah Mwangasa amewataka vijana wilayani hapa kuendelea kushikamana na kuachana na makundi jambo ambalo litaifanya Uvccm kuwa imara na kukisaida chama kupata viongozi wenye ushawishi kwa Taifa Tanzania.