Keifo FM

Kyela DC yang’ara ukusanyaji mapato

6 June 2024, 5:32 pm

Pichani ni baadhi ya wajumbe waliohudhuria kikiao hicho cha baraza la hoja ambalo limeketi katika ukumbi wa mikutano wa halmashaurri ya Kyela picha kutoka chumba cha habari

“Itakuwa haina maana kama mnaweza kukusanya fedha yote inayozidi harafu mkashindwa kutekeleza miradi ya maendeleo ya wananchi ili nao waone umuhimu wa kutoa ushuru”

Na Masoud Maulid

Mkuu wa mkoa wa mbeya Comred Juma Homera ameipongeza halmashauri ya wilaya ya kyela kwa kuvunja rekodi ya ukusanyaji wa mapato na kumuagiza mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya kyela kuzipeleka fedha hizo kwa wananchi.

Pongezi hizo zimekuja kufuatia halmashauri ya Kyela kufanikiwa kukusanya fedha jumla ya shilingi bilioni tano milioni mia tano na tisa sawa na asilimia miamoja na kumi na tatu katika makadilio ya shilingi bilioni nne milioni mia nane arobaini na tisa ya makadilio waliojiwekea.

Akizungumza akiwa katika baraza la madiwani la kujibu hoja lililokaliwa katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya kyela Homera amesema kutokana na mafanikio hayo waliyoyapata amemtaka mkurugenzi Flora Luhala pamoja na watalaamu kuzipeleka fedha hizo kwa wananchi ili waendelee kuona umuhimu wa kutoa ushuru.

Sauti ya mkuu wa mkoa wa mbeya 1

Ameongeza kwa kuwataka wataalamu kuhakikisha kiasi cha fedha jumla ya shilingi milioni miamoja na arobaini na nne za mwaka 2022-2023 ambazo hazijapelekwa benki kuhakikisha zinapelekwa benki pamoja na asiliamia arobaini za miradi ya maendeleo.

Sauti ya homera kuhusu fedha ambazo hazijakusanywa

Kuhusu ujenzi wa barabara ya Ibanda-Itungi mpaka bandari ya Kiwira hapa wilayani kyela mkuu wa mkoa wa Mbeya Juma Homera amesema mpaka sasa serikali imevunja mkataba na mkandarasi wa kwanza ambapo sasa serikali inaendelea na hatua ya kumtafuta mkandarasi mwingine ambaye atajenga barabara hiyo kwa muda mfupi.

Sauti ya mkuu wa mkoa mbeya kuhusu barabara

Akimkaribisha katibu mpya wa chama cha mapinduzi Ccm wilaya ya Kyela Deus Bidogo Homera amemsihi kuwa mtulivu wakati akiendelea kutekeleza majukumu yake ili kuhakikisha ilani ya chama cha mapinduzi inatekelezwa kwa viwango vikibwa sawa na takwa la Raisi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania.

Sauti ya mkuu wa mkoa kuhusu nasaha zake kwa katibu mypa

Katika mwaka wa fedha wa 2022-2023 halmashauri ya wilaya ya kyela ilikuwa na jumla ya hoja 38,kati ya hoja hizo kumi zilikuwa hoja za nyuma lakini hoja 28 ni za mwaka 2022-2023 kati ya hoja zote hizo hoja 21 zilikuwa zimeshatekelezwa na kufungwa lakini hoja kumi na saba zilikuwa katika hatua mbalimbali za utekelezaji.