Keifo FM

Kyela:Samia Mgeni rasmi maridhiano day Mbeya

3 February 2024, 16:31

Pichani ni damu iliyotolewa na wanafunzi wa shule za Kafundo sekondari na Ipinda sekondari wakati wa zoezi la uchangiaji damu kuelekea siku ya maridhiano day Picha na Masoud Maulid

Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania dokta Samia Suluhu Hasan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika siku ya mamaridhiano day itkayofanyika machi 3 2024 mkoani Mbeya.Na Masoud Maulid

Kuelekea siku ya maadhimisho ya Maridhiano day yatakayofanyika march 3.2024 kamati ya maridhiano na amani wilaya ya kyela imehamasisha uchangiaji damu kwa hiari na kupata mwitikio mkubwa kutoka makundi mbalimbali.

Akizungumza na mwandishi wa habari mwenyekiti wa kamati hiyo Seth Mwaisaka amesema kutokana na agizo la kamati ya maridhiano mkoa wa mbeya kuzitaka kamati za wilaya zinahamasisha wananchi kuchangia damu kwa hiari kuelekea maadhimisho hayo.

Amesema kamati ya wilaya imeanza zoezi hilo kwa kuhamasisha wanafunzi wa shule za sekondari ya ipinda na kafundo sekondari kuchangia kwa hiari ambapo mwitikio umekuwa mkubwa.

Sauti ya Mwenyekiti wa kamati ya Maridhiano wilaya ya Kyela Seth Mwaisaka kuhusu zoezi lilivyofanikiwa.
Pichani ni Mwenyekiti Seth Mwaisaka na mjumbe Ibrahimu Mwakabuli wa Kamati ya maridhino wilaya ya Kyela wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa zoezi la uchangiaji damu kuelekea siku ya maridhiano day kitaifa.

Mwaisaka ameongeza kuwa malengo ya kila kamati kutoka wilaya zote mkoa wa mbeya ni kuhakikisha ifikapo tarehe ya maadhimisho iwe tayari imekusanya damu uniti hamsini  ambapo kwa mkoa mzima wa mbeya zipatikane uniti mia tatu,hivyo kutokana na uhitaji kuwa mkubwa ameiomba jamii kupitia makundi mbalimbali kujitokeza kuchangia  ili kupata kiwango kingi cha damu salama.

Sauti ya Seth Mwaisaka akiwaomba wananchi kuendelea kujitokeza katika kujitolea kwenye zoezi la uchangiaji damu

Kwa upande wake mjumbe wa kamati hiyo Ibrahim Mwakaburi,amewapongeza Walimu na Wanafunzi wa shule hizo mbili kwa kujitokeza kuchangia kwa hiari ili kuwasaidia wahitaji,wakiwemo akina mama wanaopoteza damu nyingi wakati wa kujifungua,hivyo amewaasa wananchi  makundi ya waendesha bodaboda,mashabiki wa simba na yanga pamoja na taasisi za kidini kuwa tayari kuchangia kwa hiari zoezi litakapofika kwenye maeneo yao

Nao wanafunzi wa shule ya kafundo sekondari na ipinda sekondari  wamesema,wamejitolewa kutoa damu kwa hiari kutokana na kupata elimu kutoka kwa wataalamu  juu ya umuhimu wa kuchangia damu na kuongeza kuwa,wamekuwa wakifanya zoezi hilo mara nyingi wanapohitajika na hakuna madhara yoyote wanayoyapata baada yakuchangia damu

Sauti ya wanafunzi wakati watoji damu katika shule zao na jinsi walivyofurahishwa na zoezi hilo

Jumuia ya maridhiano na Amani imeanzishwa kitaifa mwaka 2016 mwezi march hivyo kila mwaka hufanyika amaadhisho ambapo kitaifa mwaka huu yatafanyika jijini mbeya na mgeni rasmi ni Rais wa Jamhuri ya muungano wa tanzania Dr Samia Suluhu Hasan