Keifo FM

Waathirika wa mafuriko Kyela washikwa mkono na Babylon

17 April 2024, 14:43

Pichani ni mwakilishi wa mkurugenzi wa kiwanda cha mafuta cha Covenant Edible Oil Frank Mwakapala akikambidhi mkuu wa wilaya ya Kyela chakula na mafuta ya kupikia kwa ajili ya wahanga wa mafuriko. Picha na Emmanuel Jotham.

Mkuu wa Wilaya ya Kyela Josephine Manase amemmwagia sifa mkurgenzi wa kiwanda cha mafuta ya kupikia cha Covenant Edible Oil oili Babylon Mwakyambile kwa kuwa wa kwanza kutoa misaada kwa wahanga wa mafuriko.

Na Emmanuel Jotham

Mkuu wa Wilaya ya Kyela Josephine Manase amemshukuru mkurugenzi wa kiwanda cha Covenant Edible Oil Babylon Mwakyambile  kwa kuwa mtu wa kwanza kuitikia wito wa kuwachangia wananchi waliokumbwa na mafuriko sehemu mbalimbali hapa wilayani Kyela.

DC Manase amesema kuwa kutokana na wananchi wengi kukumbwa na mafuriko na vyakula vyao kusombwa na maji, kupitia kitengo cha maafa wilaya wameanzisha mpango wa  kuwatafuta  wadau wa maendeleo wilaya ya Kyela ambapo amesema Babylon amekuwa mtu wa kwanza kuitikia wito huo.

Sauti ya DC w Kyela Josephine Manase akimshukuru mkurugenzi wa kiwanda.

Katika hatua nyingine DC Manase ametumia nafasi hiyo kuwaomba wadau wengine kuwachangia wananchi waliokumbwa na mafuriko, ikiwa ni njia sahihi ya kuwafariji wananchi hao waliofikwa na majanga hayo.

Sauti ya DC Manase akiwamomba wadau wengine wa maendeleo.

Kwa upande wake mwakilishi wa mkurugenzi wa kiwanda cha  Covenant Edible Oil Frank Mwakapala amekabidhi debe kumi za mahindi, ndoo za mafuta ya kupikia plastiki tano, ikiwa ni jitihada za kuwafariji wahanga wa mafuriko wilayani Kyela.

Sauti ya Frank Mwakapala akikabidhi chakula

Frank amemaliza kwa kutoa wito kupitia kitengo cha maafa wilaya kutosita kurudi kwa Babylon tena pale patakapokuwa na uhitaji ili kuendelea kutoa faraja kwa wahanga wa mafuriko.