Keifo FM

Nyani aingia ndani na kumjeruhi mtoto Kyela

8 March 2024, 16:09

Picha, Masud Maulid ,nyani akiwa ameuliwa na wananchi Na Masud maulid

Katika hali isiyokuwa ya kawaida nyani aina ya ngedere akiwa anakimbizwa kutoka sehemu nyingine kwenda sehemu nyingine gafla akikimbilia ndani na baadaye kumjeruhi mtoto.

Na Masud Maulid

nyani aliyekuwa anakimbizwa na watoto maeneo ya Majoka wialayni kyela  ameingia ndani ya nyumba  na kumjeruhi mtoto wa kiume anaesoma darasa la sita na kukimbizwa hospitalini kwa ajili ya matibabu.

Nyani huyo baada ya kuona kundi la watu wengi aliamua kupanda juu nyumba na kujificha juu ya dali na kukaa huko kwa takriban saa mbili, kabla ya watu kupanda juu wakiwa na silaha mbalimbali likiwemo panga.

Baada ya muda mchache yale nyani akiwa anajiandaa kushuka ndipo akakutana na motto  na kumjeruhi katika baadhi ya mwili wake na baada ya tukio hilo nyani aliweza kuuliwa na kundi la watu wakio kuwepo karibu na  eneo hilo.

Jeshi la polisi limepewa taarifa, na kushauri kuwa taarifa  wapewe wa tu wa  maliasili ambao ndio wahusika wakuu wanao pambana na wanyama kwenye maeneo mbalimbali.

Baada ya taarifa kufikishwa kwa maafisa maliasili walisema ni vyema watu wakae mbali kidogo na eneo hilo  ili nyani akiona utulivu  atashuka mwenyewe baada ya kusikia ukimya.