Madaktari wa Mama Samia watua Kyela
15 May 2024, 10:09
Wakati serikali ikiendelea na mkakati kabambe wa kuwapatia huduma za kibingwa wananchi wake timu ya madaktari bingwa watano kutoka Dar es salaam wametia nanga katika hospitali ya wilaya ya kyela kwaajiri ya huduma za kibingwa.
Na James Mwakyembe
Timu ya madaktari bingwa wa magonjwa mbalimbali ya binadamu maarufu kama madaktari wa Mama Samia imetua rasmi ndani ya wilaya ya kyela na kupokelewa katika hospitali ya wilaya na mkuu wa wilaya Josephine Manase
Madaktari hao bingwa wanatua hapa wilayani kyela ikiwa ni muendelezo wa serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania chini ya Raisi Samia Suluhu Hasan wa kushusha huduma za kibingwa kwa wananchi wake lengo likiwa ni kupunguza gharama za matibabu kwa watanzania wenye shida mbalimbali za magonjwa.
Akizungumza mara baada ya kuwapokea katika hospitali ya wilaya Mkuu wa wilaya ya Kyela Josephine Manase amemshukuru Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dokta Samia Suluhu Hasan kwa kuwatuma madaktari hao bingwa hapa wilaya ni kyela pamoja na kuwataka wanakyela kutumia vizuri fursa hiyo iliyotolewa na Rais.
Pia amewataka watumishi wa hospitali ya wilaya ya Kyela kushirikiana na madaktari hao vizuri katika kila hatua ili kubadirishana uzoefu wa kitabibu utakaokuwa endelevu kwa wananchi wilayani hapa na taifa kwa ujumla.
Akizungumza kwa naiaba ya timu ya madakatari hao bingwa wa mama Samia dokta Israel Soko daktari bingwa wa magonjwa ya kike na afya ya uzazi amesema timu hiyo inaundwa na madaktari watano ambao watakuwepo wilayani kyela kwa siku tano ambapo zitatolewa huduma za kibingwa kama ilivyo dhamira ya serikali ya kuwapatia huduma za kibingwa wananchi wake.
Kwa upande wa wananchi wilayani hapa wao wametoa pongezi kwa Raisi Mama Samia Suluhu Hasani kwa kutambua kuwa wako watanzania wa hali ya chini walio na uhitaji wa uduma za kibingwa na kuona vema kuwatuma madaktari hao katika kipindi muafaka na kumuomba raisi kuwa huduma hizi ziwe endelevu katika vipindi vijavyo.
Timu hiyo ya madaktari bingwa kutoka serikalini maarufu kama madaktari wa Mama Samia itakuwa kyela kwa muda wa siku tano ambapo huduma zitakazotolewa ni pamoja na mogonjwa ya watoto,magonjwa ya kina mama,upumuaji,ganzi na usingizi.