Keifo FM

Kyela: Sababu ya wanafunzi wengi kuachana na masomo ya sekondari  na kutimkia vyuo vya kati zatajwa

7 March 2024, 15:26

Picha,Mkufunzi mwaifunga akiwa studio za keifo fm kwenye kipindi cha asubuhi(morning Power)

Wazazi na walezi wilayani kyela wametakiwa kuwaendeleza watoto wao na masomo ya kidato cha tano ili kupata elimu bora itakayowasadia pindi watakapo maliza masomo ya ya juu tofauti na ilivyosasa wanapokimbilia vyuo vya kati.

Na Emmanuel Jotham

Akizungumzia wimbi hilo mkufunzi na mkuu wa shule ya sekondari ya keifo mpoki chata mwaifunga amesema kuwa wanafunzi wengi wanafanya hivyo kwa kuwa wanaona vyuo vya kati vinasogeza haraka kupata ujuzi wa ajira baada ya kupoteza muda wa miaka miwili sekondari,na wakihitimu wanalazimika kusoma tena  astashahada miaka miwili.

Amesema kumekuwa na wimbi kubwa la wazazi kupeleka wengi kupeleka watoto wao vyuo vya kati sababu kubwa ikitajwa kuwa ni kupunguza gharama za kusomesha watoto wao.