Keifo FM

Kyela: Wiki ya sheria yazinduliwa rasmi wilayani Kyela

26 January 2024, 23:18

Pichani ni Jopo la Mahakimu kutoka mahakama mbalimbali hapa wilayani Kyela wakiongozwa na hakimu mkazi mahakama ya Mwanzo Kyela Nasri Msafiri wakati wa zoezi la utoaji elimu ya wiki ya sheria shule ya sekondary Mwakilima Katumbasongwe Picha ba James Mwakyembe

Kuelekea kilele cha maadhimisho ya Sheria hapa nchini wanafunzi zaidi ya miatatu pamoja na walimu wao katika shule ya sekondari Mwakilima wamepatiwa elimu ya masuala mbalimbali yahusuyo haki za kisheria.

Na Nsangatii Mwakipesile

Maadhimisho ya wiki ya sheria hapa nchini Tanzania yamezinduliwa rasmi hapa wilayani Kyela kwa timu ya viongozi wa mhimiri huo muhimu katika utoaji haki wakizindua wiki hiyo katika shule ya sekondari ya Mwakilima iliyopo kata ya Katumbasongwe.

Akizungumza mara baada ya kukamilika kwa zoezi la utoaji elimu kwa walimu na wanafunzi wa Mwakilima sekondari hakimu mkazi wa mahakama ya mwanzo Kyela Mjini Nasri Msafiri amesema huo ni utaratibu wa mahakama nchini ikiashiria kuanza rasmi kwa mwaka wa mahakamahapa nchini Tanzania.

Pamoja na hayo hakimu makazi huyo wa mahakama ya mwanzo kyela mjini amesema takribani shule tano zimekusudiwa kufikiwa katika wiki hii ya sheria huku akitanabaisha kazi za mahakama katika wiki hii pamoja na kuwataka wananchi wote kujitokeza kwa wingi siku ya kilele ambayo ni tarehe 1 february 2024 katika viwanja vya mahakama ya wilaya ya Kyela.

Sauti ya hakimu mkazi mahakama ya mwanzo kyela mjini Nasri Msafiri akizungumzia kuhusu wiki ya sheria hapa wilayani Kyela

Kwa wake Justin Sailas ambaye ni afisa ustawi wa jamii hapa wilayani Kyela akiwa ameongozana na timu hiyo ya wataalam wa sheria amesema elimu hiyo imekuwa na matokeo chanya kwa kuwa imekuwa ikipunguza kwa kiasi kikubwa masuala ya matukio ya ukatili katika jamii ya wanakyela.

Sauti ya Justin Sailas afisa ustawi wa jamii wilaya ya Kyela akizungumzia namna zoezi hilo lilivyoendeshwa na jinsi lilivyo msaada kwa jamii

Kwa upande wa walimu waliopatiwa elimu ya sheria wao wamepongeza mpango huo wa mahakama na kuwaomba kuwapa nafasi karibu kila mwaka ili waweze kujua mambo mbalimbali yahusuyo sheria miongoni mwao kwani elimu hiyo inatarajiwa kuwa mkombozi katika kazi yao.

Sauti ya mwaalimu Juhudi kasanga akizungumzia namna alivyoyapokea mafunzo hayo

Wakizungumza kwa niaba ya wanafunzi wenzao katika shule ya Mwakilima Lasto Masawe na Frida Mwakilima wao wamesema wameipokea vizuri elimu hiyo ambayo wamesema kuwa itakuwa chachu kubwa ya kuongeza ufauru katika masomo yao

Sauti ya wanafunzi mwakilima wakizungumzia namna mafunzo yalivyomazuri
Picha ya wanafunzi wa sekondari ya Mwakilima wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa zoezi la elimu ya wiki ya sheria.

Wiki ya sheria imekuwa ikiadhimishwa kuanzia taraehe 24 January ya kila mwaka ambapo kilele chake hufanyika February 1 kila mwaka ikiwa ni kiashiria cha kuanza rasmi kwa mwaka mpya wa mahakama hapa nchini ambapo takribani shule tano za sekondari zinatarajiwa kufikiwa na watalaamu wa sheria kutoka mahakama za hapa wilayani kyela.