Keifo FM

Ikimba yalamba manoti ya Babylon Mwakyambile

6 May 2024, 13:29

Pichani ni viongozi wa chama cha Mapinduzi kata ya Ikimba wakipokea mifuko ya saruji kutoka kwa mdau wa maendeleo na mkurugenzi wa kiwanda cha kuzalisha mafuta Covenant Edible Oil Ltd wazarishaji wa mafuta ya kyela Cooking Oil na Sungold Cooking Oil Babylon Mwakyambile picha na Emmanuely Jotham

Mkurugenzi wa kampuni ya Covenant Edible Oil Ltd wazarishaji wa mafuta ya kyela Cooking Oil na Sungold Cooking Oil Babylon Mwakyambile amewataka wanachama wa chama cha mapinduzi kata ya Ikimba kushikamana ili kufanikisha ujenzi wa ofisi za chama hicho.

Na Nsangatii Mwakipesile.

Mdau wa maendeleo na Mkurugenzi wa kampuni ya Covenant Edible Oil Ltd wazarishaji wa mafuta ya Kyela cooking Oil na Sangold Cooking Oil Babylon Mwakyabile amekabidhi mifuko ya saruji yenye thamani ya zaidi ya shilingi laki nne katika ujenzi wa ofisi ya chama cha mapinduzi kata ya Ikimba wilayani Kyela.

Huu umekuwa mwendelezo wa mdau na Mkurugenzi huyo wa kiwanda cha kazarisha mafuta cha Kyela Cooking Oil kuendelea kushiriki na kuchangia katika shughuli mbali mbali za kijamii hapa wilayani Kyela.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wakati wa kukabidhi saruji hiyo Frank Mwakapala ambaye ni muwakirishi wa mkurugenzi wa kiwanda cha Covenant Edible Oil Ltd amewapongeza wanachama wa chama cha mapinduzi kata ya Ikimba kwa wazo hilo la kuanzisha ujenzi huo ambao utakua ni alama kwa vizazi vijavyo na kuwataka vijana wengine wa Ikimba kuchangia chama chao.

Sauti ya kaimu muwakirishi wa Mkurungenzi Frank Mwakapala akikabidhi mifuko ya saruji katika kata ya Ikimba.

Kwaupande wa katibu mwenezi wa kata ya Ikimba Mrisho Mwasele amemuomba Mwakyambile kuendelea kuwasaidia katika ujenzi huo kwasababu mchakato huo wa ujenzi umeanza tangu Mwaka 2006 ujenzi ambao ulikwama kukamilika kwa wakati kutokana na kukosekana kwa rasilimali fedha na hivyo kumuomba kuwasaidia kukamilisha jengo hilo ili liweze kutumika kwa shughuli mbalimbali za kichama.

Sauti ya katibu mwenezi wa kata ya Ikimba Mrisho Mwasele akimuomba Mwakyambile Ela ya ujenzi wa ofisi hiyo.

kwa upande wa viongozi wachama cha mapinduzi  kata ya Ikimba wamemshukuru Babylon Mwakyambile kwa mchango wake huo kwani kuna wadau wengi waliowaomba na mpaka sasa bado hawajawaunga mkono tofauti na yeye aliyelipa uzito ombi lao.

Sauti ya viongozi wa kata ya Ikimba wakimshukuru Babylon Mwakyambile.
Pichani ni baazi ya wananchi wa kata ya Ikimba waliojitokeza wakati wa kupokea saruzji hizo kutoka kwa madau huyo wa maendeleo

Hii si mara ya kwanza kwa mdau huyo wa maendeleo na Mkurugenzi wa kampuni ya Covenant Edible Oil Ltd wazarishaji wa mafuta ya Kyela Cooking Oil na Sangold Cooking Oil kushiriki katika kuchangia shughuli mbalimbali za kijamii hapa wilayani kyela kwani mpaka sasa amekwisha fanya hivyo katika kata za Isaki,Ngusa,Itunge,Kajunjumele,Ikimba na ofisi za chama wilaya ya kyela ambapo ameahidi kuendelea kushikamana nao katika kila hali.