Keifo FM

Kyela: Bablon kuishi na maono ya wototo yatima

23 December 2023, 16:01

Pichani ni Bablon Mwakyambile akiwa amejihudhurisha mbele ya Mungu Mkuu wakati wa ibada ya kukabidhi misaada kwa watoto yatima 36. Picha na Nsangatii Mwakipesile

Mdau wa maendeleo wilayani Kyela Bablon Mwakyambile ametoa misaada mbalimbali ikiwemo fedha taslimu shilingi laki tano kwa watoto yatima 36 huku akiahidi kuendelea kuwakumbuka katika mambo mengine.

Na James Mwakyembe

Ibada ya kuwatunza watoto yatima 36 imefanyika katika kanisa la Baptist wilayani Kyela na kuhudhuriwa na mdau wa maendeleo na mgeni rasmi Bablon Anderson Mwakyambile wa ibada hiyo maalumu.

Kizungumza katika Ibada hiyo Mwakyambile amewataka watoto hao kujituliza na kutokuhofia kukosekana kwa wazazi wao kwani hata sasa wao ni sehemu ya wazazi waliotayari kuwatunza kikamirifu pasina shaka yoyote.

Sauti ya Bablon Mwakyambile wakati akitoa neno la faraja kwa watoto yatima

Akikabidhi fedha tasrimu shilingi laki tano kwa niaba ya familia mke wa Bablon Mwakyambile amesema mpaka sasa wao kama sehemu ya familia hiyo mpya wataendelea kuwa nayo sambasamba na kumuomba Mwalimu Mwakibinga kuangalia maeneo mengine yenye uhitaji ili kushirikiana nao hasa katika eneo la elimu.

Sauti ya Mke wa Bablon akizungumzia kiwango kilichotolewa na familia
Pichani ni familia ya Bablon Mwakyambile wakiwa katika picha ya pamoja kanisani hapo

Akizungumza kwa niaba ya watoto hao waliopokea misaada hiyo kutoka kwa mdau huyo Bablon Mwakyambile mchungaji wa kanisa la Baptist Kyela mjini Dikson Mwankanda amemshukuru mwakyambile kwa moyo aliouonesha kwa watoto hao na kumuomba kuendelea kuwa pamoja nao.

Sauti ya Mchungaji Dikson Mwankanda akitoa neno la baraka kwa familia ya Bablon Mwakyambile

Ibada hiyo ya kuwapatia misaada watoto yatima imefanyika ikiwa ni muendelezo wa ibada zingine nyingi zilizotangulia katika miaka iliyopita ambapo vitu mbalimbali vimeweza kutolewa ikiwemo mavazi na chakula.