Keifo FM

Milioni kumi na tano zamwangwa kukarabati machinjio ya Mikoroshoni

27 November 2023, 19:10

Gwakisa Mwakipesile-Diwani wa kata ya Mikoroshini.Picha na James Mwakyembe

Jumla ya shilingi milioni kumi na tano zimetolewa na serikali ya awamu ya sita kwaajiri ya ujenzi wa miundombinu ya machinjio ya kisasa hapa wilayani Kyela.

Na James Mwakyembe

Wakati serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikiendelea kuboresha miundombinu ya kijamii hapa nchini Diwani wa kata ya Mikoroshoni Gwakisa Mwakipesile amemshukuru raisi Samia Suluhu Hassani kwa kutoa fedha zilizofanikisha ujenzi na ukarabati wa machinjio ya kisasa katika kata yake hapa wilayani Kyela.

Haya yanajiri ikiwa imepita miaka kumi tangu machinjio hiyo ikumbwe na kadhia ya kufungwa na mamlaka husika kutokana na kukosa hadhi ya kuendelea kutoa huduma ya machinjio hali iliyosababisha usumbufu mkubwa kwa walaji wa nyama hapa wilayani.

Akizungumza na kituo hiki Mwakipesile amesema jumla ya shilingi milioni kumi na tano zimetumika katika kukarabati miundombinu ya machinjio hiyo ambayo amekiri kuwa imekuwa mkombozi kwa vijana na wakaazi wengi waliokuwa wamekosa ajira.

Sauti ya Gwakisa George diwani Mikoroshini

                   

Kuhusu juhudi za usafi na utunzanji wa mazingira ya machinjio amesema uongozi wa kata chini ya mtendaji wake waliitisha vikao vya kutoa elimu ya kutunza miundombinu ya machinjio hiyo ili kuhakikisha usalama unapatikana na kuifanya idumu zaidi.

Sauti ya Gwakisa George diwani wa Mikoroshini

             

Akizungumzia kuhusu mifereji ambayo awali ilikuwa ikitiririsha maji katika maeneo yanayozunguka makazi ya watu na kusababisha usumbufu mkubwa kwa wananchi wanaozunguka machinjio hayo amesema tayari kero hiyo imetatuliwa kwa kujengwa mashimo makubwa yanayohifadhi taka zote zinazozarishwa eneo hilo.

Sauti ya Mwakipesile

Mwakipesile amehitismisha kwa kuwataka wananchi wa kata ya Mikoroshoni kuendelea kumuamini na kuiamini serikali ya awamu ya sita chini ya raisi mpamabanaji Samia Suluhu Hassani ili aendelee kuzitatua kadhia zinazoikumba kata hiyo ikiwemo ujenzi wa barabara za lami unaotarajiwa kuanza kutekelezwa katika siku za usoni.