Keifo FM

Mwamengo atoa mkono wa faraja kwa watoto yatima 36 wilayani Kyela

23 December 2023, 14:49

Piachani ni Mkurugenzi wa General Supplies Limited Baraka Mwamengo alipoalikwa kama mgeni rasmi kwenye ibada ya kukabidhi misaada kwa wototo yatima 36 kanisa la Baptist Kyela mjini.

Mkurungenzi wa kampuni ya ujenzi ya Basai General Supplies Limited Baraka Mwamengo ametoa jumla ya shilingi laki nane kwa watoto yatima 36 wanaolelewa na familia ya mwalimu Mwakibinga hapa wilayani Kyela.

Na James Mwakyembe

Kuelekea sikukuu za mwisho wa mwaka za Krismas na mwaka mpya watoto 36 wasio na wazazi hapa wilayani Kyela wamepatiwa na misaada na waumini mbalimbili wa dini ya Kristo hapa wilayani kyela ikiwa nisehemu ya kuwafariji watoto hao.

Akizungumza sababu za kutoa misaada hiyo mbele ya mgeni rasmi Baraka Mwamengo kutoka kampuni ya ujenzi ya Basai mwalimu Mwakibinga amesema sababu ni kuwa watoto hao wanahitaji faraja kutoka kwa jamii inayowazunguka kama vitabu vitakatifu vinavyosema.

Sauti ya Mwalimu Mwakibinga akitoa taarifa ya watoto yatima mbele ya Mgeni rasmi Baraka Mwamengo

Kwa upande wa mchungaji wa kanisa la Baptist wilaya ya Kyela Diksoni Mwankanda amesema kitendo hicho cha mwalimu mwakibinga ni sadaka kubwa mbele za Mungu hivyo kuwashukuru watu wote walishiriki katika ibada hiyo ya faraja kwa watoto hao.

Sauti ya mchungaji Mwankanda wa kanisa la Baptist Kyela mjini akielezea juu ya nafasi ya kuwathamini watoto yatima

Akizungumza katika ibada hiyo maalumu ya kuwafariji watoto hao mgeni rasmi katika ibada hiyo Baraka Mwamengo amewapongeza familia ya mwalimu Mwakibinga kwa  maono hayo ya kuwafariji watoto hao na kuwataka kuendelea mbele zaidi kuwakusanya watoto zaidi.

Sauti ya Baraka Mwamengo akitoa shukrani zake kwa familia ya mwalimu Mwakibinga
Pichani ni watoto 36 yatima waliopatiwa mahitaji muhimu kanisani na Baraka Mwamengo

Kuhusu watoto Mwamengo amewataka watoto hao kujiona kama wazazi wanaishi na hivyo kujikita zaidi katika kufanya vizuri kwenye masomo yao ili kuhakikisha wanatimiza ndoto zao huku akiahidi kuendelea kuwa pamoja nao katika mwaka ujao ambapo ametoa shilingi laki nane kama sehemu ya kuwatia faraja watoto hao

Sauti ya Baraka Mwamengo kutoa fedha na kuwataka kusoma kwa bidii
Baraka Mwamengo akiwa katika kanisa la Baptist Kyela mjini

Sambamba na hilo Mwamengo ameahidi kutoa tripu nne za mchanga pamoja na saruji mifuko hamsini kuchangia ujenzi wa kanisa hilo lililopo kyela mjini pamoja na kutengua naziri yake kwa kanisa lingine lililopo Mwanjabala kiasi cha shilingi laki tatu ambacho amekikabidhi kwa mchungaji Dikson Mwankanda kutokana na kubwanwa na muda.