Keifo FM

Kyela:Milioni mbili zatolewa na tunajivunia Kyela Yetu kwa shule nne Kyela

9 January 2024, 21:25

Picha ya pamoja ya wanaumoja wa kikundi cha tunajivunia Kyela yetu wakiwa na baadhi ya vifaa vya kukabidhi katika shule ya msingi Kasumulu picha na Nsangatii Mwakipesile

Watoto zaidi ya sabini wenye uhitaji maalumu wamepokea vifaa mbalimbali vya kujifunzia kutoka kwa umoja wa kikundi cha tunajivunia Kyela Yetu hapa wilayani Kyela.

Na James Mwakyembe

Vifaa mbalimbali vya kujifunzia vyenye thamani ya shilingi milioni mbili vimetolewa na umoja wa kikundi cha Tunajivunia Kyela Yetu katika shule za msingi nne hapa wilayani kyela kwa watoto wenye uhitaji maalumu.

Vifaa hivyo vimetolewa na umoja wa tunajivunia Kyela yetu inayounganisha wadau mbalimbali wa maendeleo wanaopatikana ndani na nje ya Kyela lengo likiwa ni kuwasogeza watoto hao karibu na jamii licha ya mapungufu walinayo.

Akikabidhi vifaa hivyo mbele ya kaimu afisa elimu msingi Jofrey Paulo ambaye ni afisa elimu ya watu wazima hapa wilayani kyela mwenyekiti wa jamii wa tunajivunia kyela yetu Vanesa Ngesienge akiwakirisha viongozi wake amesema vifaa hivyo vimegharimu jumla ya shilingi milioni mbili fedha zilizotolewa na wadau mbalimbali wanaounda umoja huo.

Sauti ya Vanesa Ngesienge mwenyekiti wa jamii tunajivunia kyela yetu kuhusu vifaa
Sauti ya Vanesa Ngesienge mwenyekiti wa jamii tunajivunia kyela yetu kuhusu vifaa
Pichani ni baadhi ya watoto katika shule ya msingi Kasumulu wakiwa pamoja na wanakikunda cha tunajivunia Kyela yetu na vifaa vilivyokabidhiwa

Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa vifaa hivyo afisa kaimu afisa elimu msingi hapa wilayani Kyela Jofrey Paulo amesema shule hiyo inayo wahitaji wengi hali inayopelekea watoto hao kushindwa kupata elimu bora hivyo kuwashukuru Tunajivunia Kyela yetu na kuwataka kuendelea hivyo katika Nyanja zingine.

Sauti ya kaimu afisa elimu msingi Jofrey Paulo akitoa shukrani kwa tunajivunia kyela yetu

Wakipokea vifaa hivyo kutoka kwa kaimu afisa elimu mwalimu mkuu wa shule ya Kasumulu Mwanahawa Nguzo pamoja na mwalimu Tusajigwe Mwangomile ambaye ni mwalimu wa elimu maalumu wameshukuru msaada huo ambao wameutaja kuwa sehemu ya kupunguza uhitaji walionao shuleni hapo kwa watoto hao.

Sauti ya mwalimu mkuu Kasumulu mwanahawa Nguzo pamoja na tusajigwe mwangomile mwalimu elimu maalumu wakitoa shukrani kwa tunajivunia kyela yetu

Umoja wa kikundi cha Tunajivunia Kyela Yetu ulianzishwa kupitia mtandao wa kijamii wa whatsap tarehe 28 Ogasti 2021 likiwa na lengo la kusaidiana katika shida na raha jambo ambalo sasa limevuka mpaka kuifikia jamii ya wanakyela kusaidia watu mbalimbali wenye uhitaji.