Keifo FM

Maandamano ya CHADEMA yanukia Kyela

18 March 2024, 13:12

Pichani ni ofisi za chama cha demokrasia na amaendeleo CHADEMA wilaya ya Kyela Picha na Nsangatii Mwakipesile

Wanachama na makada wa CHADEMA wilaya ya Kyela wanajipanga kufanya maandamano makubwa ya amani kushinikiza serikali kuunda tume huru ya uchaguzi.

Na James Mwakyembe

Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA wilayani Kyela kupitia katibu wake mwenezi Donald Mwaisango kimesema kinajipanga kufanya maandamano makubwa hapa wilayani Kyela huku akisifu uimara wa mwenyekiti mpya Victoria Swebe.

Mwaisango amesema hayo ikiwa ni siku chache zimepita tangu chama hicho kikuu cha upinzani hapa nchini Tanzania kuhitimisha maandamano yake ya amani katika majiji manne yaliyoratibiwa na CHADEMA Taifa.

Akizungumza moja kwa moja kutoka katika ofisi za chama hicho hapa wilayani kyela Mwaisango amebainisha kuwa baada ya kumalizika kwa chaguzi za ndani na maandamano ya kitaifa sasa chama hicho kinakusudia kufanya maandamano makubwa ndani ya wilaya ya Kyela yatakayoongozwa na kiongozi mmoja kutoka CHADEMA taifa.

Sauti ya Donald Mwaisango kuhusu maandamano wilaya ya Kyela siku chache zijazo.
Pichani Ni katibu mwenezi wa CHADEMA wilaya ya Kyela Donald Mwaisango

Kuhusu lini maandamano hayo yatafanyika hapa Kyela Mwaisango hajaweka wazi kuwa lini yatafanyika huku akiwaomba watanzania kushiriki katika maandamano hayo ya amani muda utakapofika.

Katika hatua nyingine Mwaisango amesema chama hicho kiko imara chini mwenyekiti wao mpya Victoria Swebe aliyechaguliwa hivi karibuni ambapo ametumia muda huo kuwataka wanachama wake kupuuza habari zozote wanazozisikia juu ya kamati kuu ya chama hicho wilaya.

Sauti ya Mwaisango kuhusu uimara wa chama hicho chini victoria swebe.

Kazarika akatoa kalipio kali kwa viongozi wa chama hicho ngazi za kata kuwa wajiweke tayari kwa ajiri ya kupokea na kutekeleza maagizo ya chama mara moja na kuwa kama chama hawatakuwa na uvumilivu kwa kiongozi yeyote ambaye hatatekeleza wajibu wake ipasavyo.

Sauti ya Mwaisango kuhusu kalipio kubwa kwa viongozi wa chama ngazi ya kata.

Amehitimisha kwa kuwataka viongozi wa chama hicho kuendelea kushikamana na kutafuta wanachama wapya ili kukijenga chama hicho ambapo amesema hivi karibuni wanakusudia kufanya ziara ya kata kwa kata lengo likiwa ni kukiimarisha chama.