Keifo FM

Kyela:Samia atua rasmi Kyela

4 January 2024, 12:45

Picha ya wanaumoja wa CHAMATA TANZANIA wilayani kyela Picha na James Mwakyembe

Wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hasan akiendelea kutekeleza miradi mikubwa yenye fedha nyingi jukwaa la kumsemea MAMA maarufu kama CHAMATA limeanzishwa rasmi wilayani kyela na kufanya uchaguzi wa viongozi wake.

Nsangatii Mwakipesile

Umoja wa jukwaa la CHAMATA TANZANIA wilaya ya Kyela umeanzishwa rasmi na kufanya uchaguzi wake wa kwanza kuwapata viongozi wake watakaoliongoza jukwaa kwa hapa wilayani Kyela.

CHAMATA TANZANIA wilaya ya Kyela imeanzishwa ikiwa na lengo la kuwaunganisha wanakyela walio na mapenzi mema na Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hasani kupaza sauti zao kwa watanzania wenzao ili kuzisemea kazi zilizotukuka za mama kwa watanzania.

Akizungumza baada ya zoezi la uchaguzi kukamilika mwenyekiti wa CHAMATA mkoa wa Mbeya Mpeli Mwakyembe amesema kazi kubwa ya CHAMATA ni kupaza sauti yao kuyasema mambo makubwa yanayofanywa na Mama Samia Suluhu Hasani Rais wa Tanzania ambayo wapo baadhi ya wanasiasa wanaotumia muda wao kupatosha watanzania.

Sauti ya Mpeli Mwakyembe Mwenyekiti CHAMATA mkoa wa Mbeya
Pichani ni mwenyekiti CHAMATA Mkoa wa Mbeya Mpeli Mwakyembe

Akitangaza matokeo ya uchaguzi wa CHAMATA wilaya ya Kyela msimamizi wa uchaguzi huo Joseph Lubida amewapongeza waliochaguliwa na kuwataka kusimamia misingi na kanuni ya jukwaa hilo ili azma yao itimie sawa na makusudio yao.

Sauti ya msimazi wa uchaguzi Joseph Lubida akitangaza matokeo ya uchaguzi

Kwa upande wa mwenyekiti aliyechaguliwa wa jukwaa hilo Wiliam Mwangomile amesema baada ya zoezi la uchaguzi kukamilika kazi yao kubwa sasa ni kuhakikisha wajumbe wa jukwaa hilo wanapaza sauti zao ipasavyo kumsemea MAMA kwa watanzania hapa wilayani Kyela.

Sauti ya Mwenyekiti mpya Wiliamu Mwangomile akishukuru kwa wajumbe
Pichani ni mwenyekiti wa CHAMATA wilaya ya Kyela Wiliam mwangomile

Kwaniaba ya wajumbe walioshiriki uchaguzi huo Ibrahimu Mwanjute amemshukuru mwenyekiti wa mkoa na kuwataka wana CHAMATA kuhakikisha wanatimiza majukumu yao ipasavyo katika maeneo mengi pamoja na kumhakikishia mwenyekiti wake ushirikiano mkubwa katika kazi zake za kila siku.

Sauti ya Ibrahimu Mwanjute akitoa neno kwa mwenyekiti mkoa wa Mbeya

CHAMATA ORGANISATION ni jukwaa rasmi lililoanzishwa na watanzania kwa lengo kumsemea MAMA Samia Suluhu Hasani katika mambo makubwa anayoyafanya ya kuwaletea wananchi wa Tanzania maendeleo.