Keifo FM

Kyela:Covenant Edible Oil yamwagiwa pongezi na mbunge jimbo la Kyela

4 April 2024, 13:29

Pichani ni Mbunge wa jimbo la Kyela Ally Mlaghila Jumbe akiwakabidhi wananchi mfano wa hundi ya fedha yenye thamani ya shilingi milioni tatu kwaajiri ya ununuzi kiwanja cha kujenga shule ya msingi Mpegele hapa wilayani kyela picha na Masoud Maulid

Baada ya mkurugenzi wa Covenant Edible Oil Ltd kufanya juhudi kubwa za kuwaletea maendeleo na fursa za ajira wakazi wilayani hapa mbunge wa jimbo la Kyela Ally Mlaghila Jumbe amempongeza mkurugenzi huyo na kuwataka wadau wengine kufuata njia hiyo ili kuiletea kyela maendeleo.

Na  Masoud Maulid

Kutokana na kazi mbalimbali za kimaendeleo zinazofanywa na wadau mbalimbali wa maendeleo wilayani hapa mbunge wa jimbo la Kyela Ally Mlaghila Jumbe amewapongeza wadau hao kwa kazi zao za kuendelea kuwasaidia wananchi wilayani hapa kwa kutoa misaada mbalimbali kwa makundi tofauti.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara katika kijiji cha mpegele kata ya makwale  mbunge huyo  amesema,moja ya ahadi zake kipindi cha kampeni ni kushirikiana na wadau wa maendeleo ndani na nje ya kyela.

Miongoni mwa wadau waliopongezwa na mbunge wa jimbo la Kyela ni mkurugenzi wa kampuni ya ujenzi wa barabara basai Baraka Mwamengo kwa misaada anayoendelea kutoa kwa wananchi wa kyela ikiwemo kutoa msaada wa madawati pamoja na  shilingi laki nane kwa kata ya makwale.

Sauti ya  kinanas kuhusu pongezi zake kwa wadau wa maendeleo hapa wilayani kyela

Pia Mlaghila amempongeza mkurugenzi wa kiwanda cha kuzalisha mafuta wilaya ya kyela Covenant Edible Oil Ltd Babylon Mwakyambile ambaye amekuwa mstari wa mbele kwa kuwasaidia wananchi ndani ya wilaya ya kyela kuwataka viongozi wengine kuendelea kumuunga mkono na kuacha hofu kwamba wanatoa misaada hiyo wakiwa na lengo la kugombea ubunge.

Sauti ya mbunge ally kuhusu pongezi zake kwa wadau tajwa hapa kyela
Mbunge wa jimbo la Kyela Ally Mlaghila Jumbe akiongea wakati akiwa katika ziara yake ya kikazi mpegele makwale hapa wilayani kyela

Katika hatua nyingine mbunge Ally Mlaghila amesema,hawezi kuwachukia wala kuwazuia wadau mbalmbali kuendelea kusaida wilaya ya kyela kwakuwa mbunge pekee aliyeko madarakani ndiye mwenye jukumu la kuandika utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi ccm.

Sauti ya  mlaghila kuhusu utekelezaji wa miradi na ilani ya chama kwa miaka mitano ijayo

Katika kujibu kilio cha wananchi wa kijiji cha mpegele kuhusu changamoto ya kukosekana shule ya msingi katika kijiji hicho,mbunge ameahidi kushirikiana na wananchi kila hatua ili kufanikisha ujenzi wa shule ya msingi huku akiunga mkono jitihada za wananchi kwa kutoa shilingi milioni tatu kwa ajili ya kununua kiwanja ambacho kinacho ghalimu kiasi cha shilingi milioni tano.

Sauti ya wananchi mpegele kuhusu kukosekana kwa shule katika kijiji hicho

Kijiji cha mpegele kata ya makwale wilaya ya kyela kwa muda mrefu kinakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa huduma mbalimbali ikiwemo huduma ya elimu pamoja na huduma za afya jambo ambalo limekuwa likiwafanya wakazi kijijini hapo kutembea umbali mrefu kufuata huduma za kijamii.