Keifo FM

Mbeya: Samia mgeni rasmi maadhimisho ya maridhiano kitaifa

8 January 2024, 16:14

Pichani ni wajumbe wa jumuiya ya maridhiano wilaya ya wakiwa katika picha ya pamoja Picha na Masoud Maulid

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania dr Samia suluhu Hasani anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika siku ya maridhiano kitaifa yanayotarajia kufanyika mkoa wa Mbeya mwezi machi mwaka huu.

Na Masoud Maulid

Kuelekea   maadhimisho ya siku ya maridhiano kitaifa march 3,2024 kamati ya maridhiano wilaya ya kyela imekusudia kuihamasisha  jamii kuchangia damu kwa lengo la kuwasaidia watu wenye uhitaji.

Akizungumza na mwandishi wa habari mwenyekiti wa jumuia ya maridhiano wilaya ya kyela seth mwaisaka amesema mwaka huu 2024 maadhimisho ya siku ya maridhiano kitaifa yatafanyika jiji la mbeya ambapo mgeni rasmi atakuwa  rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania dr samia suluhu hasani.

Mwaisaka ameongeza kuwa kabla ya siku hiyo,kamati za maridhiano mkoa wa mbeya zimepewa jukumu la kuhamasisha jamii kuchangia damu,ambapo kila wilaya kamati imetakiwa kukusanya damu unit hamsini ambazo zitabaki  hospitali katika wilaya husika ili kuwasaidia wagonjwa wakiwemo akina mama wajawazito,hivyo ameiasa jamii kuwa tayari kuchangia damu zoezi litakapoanza.

Sauti ya Mwenyekiti wa kamati ya maridhiano wilaya ya Kyela Seth Mwaisaka akizungumzia juu ya zoezi la utoaji damu

Kwa upande wake Ibrahimu mwakaburi ambaye ni mjumbe wa kamati ya maridhiano wilaya ya kyela amesema mpango wa uchangiaji damu ni jambo muhimu sana ambalo litafanikisha kuokoa maisha ya watu mbalimbali hasa akina mama wanaojifungua na madereva bodaboda wanaopata ajali,hivyo ameitaka jamii kila mmoja katika eneo lake alipokee jambo hili na kuliona ni sehemu ya uzalendo katika taifa la tanzania.

Sauti ya Ibrahimu Mwakaburi akizungumzia mpango wa jumuiya ya maridhiano wilaya ya Kyela kuchangia damu

Nae shekhe Ally Ally mjumbe wa kamati ya maridhiano yeye amesema suala la kuchangia damu halichagui  dini,kabila wala rangi bali lengo ni kuisaidia jamii hivyo ametoa wito kwa taasisi mbalimbali kulihamasisha jambo hilo kwenye taasisi na kuondoa dhana potofu kwamba kuchangia damu kuna madhara kwa  anayechangia  damu.

Sauti ya Shekhe Ally Ally akizungumza juu ya utayari wao kwenye zoezi lililombele yao ya kuhamasisha jamii ya Kyela kuchangia damu

Jumuia ya maridhiano na amani tanzania ilianzishwa march tatu mwaka 2016 kwa lengo la kudumisha amani Tanzania.