Keifo FM

Kyela:Kinanasi aungana na waislamu funga ya mwezi mtukufu

20 March 2024, 13:09

Pichani ni msikiti mkuu wa wilaya ya Kyela moja ya misiki ilipokea sadaka ya funga kutoka kwa mbunge wa jimbo la kyela Ally Mlaghila Kinanasi Picha na Masoud Maulid

Wakati waumini wa dini ya kiislamu wliayani kyela wakiendelea na mfungo wa mwezi mtukufu wa ramadhani mbunge wa jimbo la Kyela Ally Mlaghila Kinanasi ametoa sukari na mitungi ya gesi kwa kila msikiti wilayani kyela.

Na Masoud Maulid

Mbunge wa jimbo la Kyela Ally Mlaghila Kinanasi ameungana na waislamu wilaya ya kyela wanaotekeleza nguzo ya nne katika dini ya KIislamu ya kufunga mwezi mtukufu wa ramadhani kwa kutoa sadaka ya sukari na mtungi wa gesi kwa kila msikiti.

Akizungumza na mwandishi wa habari katibu wa mbunge Edger Mwasamlagila amesema zoezi la kugawa sadaka hiyo angeifanya mbunge mwenyewe  kupita kila msikiti wilaya ya kyela lakini kutokana na majukumu ya kushiriki vikao vya kamati jijini Dodoma,hivyo zoezi hilo linatekelezwa na katibu wake ambapo ugawaji wa sukari kilo 40 pamoja na mtungi mmoja wa gesi vimetolewa msikiti mkubwa wa wilaya.

Sauti ya katibu wa mbunge wa jimbo la kyela kuhusu zoezi la ugawaji sadaka katika misikiti wilaya ya kyela
Pichani Ni katibu wa mbunge Edger Mwasamlagila akikabidhi mtungi wa gesi na kilo arobaini za sukari kwa ustadhi Ayubu Haruna mjumbe wa kamati ya msikiti wa Aqswa uliopo mikumi Kyela

Mwasamlagila ameongeza kuwa zoezi la kutoa sadaka hiyo linaendelea kufanyika katika misikiti ambayo wameweka utaratibu wa kuwafuturisha waislam eneo moja la msikiti tangu kuanza kwa ramadhani,ambapo watakabidhiwa  sukari pamoja na mtungi wa gesi lengo likiwa pia ni kuunga jitihada za rais wa jamhuri ya muungano wa tanzania katika kutumia nishati mbadala  ambapo rais  ni mjumbe wa kamati.

Sauti ya edgar Mwasamlagila akizungumza kuhusu misikiti itakayopokea sadaka hiyo katika kipindi hiki cha mwezi wa ramadhani

Kwa upande wake imamu wa msikiti mkuu wa wilaya kupitia baraza kuu la waislamu Tanzania BAKWATA Omary Ngelangela,ametoa shukrani kwa niaba ya waislamu kwa sadaka ambayo imetolewa na mbunge wa jimbo la Kyela na kuahidi kuendelea kumpatia ushirikiano na kumuombea kwa mwenyezi mungu ampe afya na nguvu zaidi ya kuwatumikia wananchi wa jimbo lake.

Sauti ya Immamu omary ngelangela akitoa neno la shukrani kwa wawakilishi wa mbunge kupokea sadaka hiyo

Nae ustadhi Ayubu haruna mjumbe wa kamati ya msikiti wa Aqswa uliopo kitongoji cha mikumi kata ya bondeni amesema hawakutarajia kupa msaada huo ndani ya mwezi huu wa ramadhani hivyo wamempongeza mbunge kwa maono yake hivyo nao pia wanamuombea kwa mwenyezimungu awe na moyo wa kuendelea kuwakumbuka waislmau na katika mambo mengine

Sauti ya  ustadhi ayubu akishukuru kwa niaba ya waumini wa dini ya kiislamu msikiti wa Mikumi

Misikiti inayotaraji kupokea sadaka hiyo ya sukari kilo 40 pamoja na mtungi wa gesi ni pamoja msikiti mkuu wa wilaya,masjidi aqswa,masjidi madinatul-mnawara boda,masjidi raub`wa njisi,msikiti wa stamiko,msikiti wa makwale,msikiti wa itope,ipinda na msikiti wa tenende.