Orkonerei FM

Wanajamii wapewa elimu juu ya kujiingizia kipato kipindi cha ukame

9 July 2024, 1:35 pm

Afisa Kilimo na Mifugo kata ya Terrat Bw.Petro Mejooli Lukumay akiwa katika shamba darasa kijiji cha Terrat. (Picha kwa msaada wa mtandao.)

Na Joyce Elias.

Afisa kilimo kata ya Terrat Ndg.PETRO MEJOOLI LUKUMAY amesema kuwa wanajamii wanatakiwa kulima mbogamboga na mazao mengine mchanganyiko ili kujiingizia kipato haswa wakati wa upungufu wa mvua ama ukame.

Ametoa elimu hiyo kupitia mahojiano mafupi aliyoyafanya na mwandishi wetu JOYCE ELIUS, ambapo amesema kuwa wao kama wataalamu huwa wanapata nafasi katika mikutano ya kijamii kutoa elimu hizo ili kupambana na ukame wakati wanajamii wanajiingizia kipato.

Huyo ni Afisa kilimo akitoa elimu jinsi ya kukabiliana na ukame kipindi cha kiangazi hasa kwa wakulima na wafungaji Bw Petro Mejooli Lukumay.