Orkonerei FM

Wazazi wahimizwa kuwapeleka watoto wao shule

12 November 2024, 12:23 pm

Mkurugenzi wa Shule ya Flaherty Altapuai Thadeus pamoja na Mkazi wa Kijiji cha LoiborSoit A’ Bw Paulo Lenina.

Wazazi wa Jamii ya Wafugaji wamaasai wametakiwa kutumia mifugo walionao na raslimali zingine kuwapeleka watoto wao Shule bila kuwabagua.

Na Baraka David Ole Maika.

Wito huo umetolewa na Mkurugenzi wa Shule ya Mchepuo wa Kiingereza ya Flaherty iliyopo Kijiji cha LoiborSoit A’ Kata ya Emboret Bw Altapuai Thadeus alipozungumza na Orkonerei FM Radio.

Bw Altapuai amesema kuwa ni vema jamii wakatambua kuwa elimu ndicho kitu muhimu na cha thamani kwa watoto wao hivyo ni vema wakawapeleka watoto shule pasipo kuwabagua.

Sauti ya Mkurugenzi wa Shule ya Flaherty Bw Altapuai Thadeus

Naye mkazi wa kijiji cha LoiborSoit A’ Bw Paulo Lenina amesema kuwa huu ni wakati ambao jamii ya wafugaji wanatakiwa wabadilike na kuwekeza kwenye elimu kwani misimu imekuwa ikibadilika na hata mataifa yalioendelelea wamefikia hatua hiyo baada ya kuelewa umuhimu wa elimu kwa kuwapeleka watoto wao shule.

Sauti ya Mkazi wa kijiji cha LoiborSoit A’Bw Paulo Lenina.

Aidha Bw Paulo amesema kuwa kwa wakati huu wa mabadiliko ya tabianchi sio vema jamii ya wafugaji kuendelea kutegemea ufugaji wa mifugo wengi wasio na tija ila ni wakati wa kubadilisha mawazo kwa kuwekeza kwenye elimu kwa kuwapeleka watoto shule.

Sauti ya Mkazi wa kijiji cha LoiborSoit A’Bw Paulo Lenina.

Shule ya Msingi Flaherty ni shule ya mchepuo wa kiingereza iliyopo kijiji cha LoiborSoit A’ kata ya Emboret wilayani Simanjiro na ni shule ya bweni na kutwa kwa wasichana na wavulana.

Shule ya Msingi Flaherty.