Orkonerei FM

Mtoto wa miaka 12 aokolewa kutoka kwenye ndoa ya lazima

8 October 2024, 11:54 am

Na Isack Diskson

Licha ya sheria kukataza ndoa za utotoni, bado hali ni tete Simanjiro baada ya mtoto wa miaka 12 kuokolewa kutoka kwenye ndoa ya lazima.

Mtoto wa miaka 12 mkazi wa kata ya Oljoro No.5 wilaya ya Simanjiro ameokolewa kutoka kwenye ndoa aliyoozeshwa na walezi wake.

Akizungumza na Orkonerei FM Radio, babu wa binti huyo amesema kuwa walipata taarifa kutoka kwa baba wa binti huyo ambaye alinyimwa kumchukua mtoto wake kutoka kwa wazazi wa mama yake aliyefariki miaka 12 iliyopita mara baada ya kujifungua mtoto huyo.

Aidha baba yake mdogo na binti huyo naye aliweza kueleza jinsi baba yake alivyompa mtoto huyo kwenda kwa bibi yake.

Kwa upande wa uongozi wa tarafa ya Teerat umekiri kuwa ukatili wa kijinsia bado ni changamoto ndani ya jamii.