Karagwe FM

Recent posts

29 July 2024, 1:08 pm

Waganga wa tiba asili wadaiwa kuchochea mauaji, ubakaji Kagera

Jeshi la Polisi Mkoa wa Kagera kupitia ofisi ya upelelezi limekutana na waganga wa tiba asili na viongozi wa kimila kujadili juu ya wimbi la vitendo vya uhalifu unaohusisha mauaji ya watu wenye ualbino na ubakaji wa watoto, yote yakihusishwa…

26 July 2024, 9:19 pm

Mwenyekiti ALAT Taifa ahimiza usimamizi wa miradi ya maendeleo

Kamati tendaji ya Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania ALAT wamekutana wiki hii kujadiliana juu ya mambo mbalimbali ikiwemo kutoa maelekezo kwa mamlaka za serikali za mitaa juu ya usimamizi wa miradi ya maendeleo katika maeneo yao Na mwandishi wetu…

26 July 2024, 2:48 pm

RC Kagera asisitiza kuwaenzi mashujaa kwa kudumisha amani

Kila ifikapo Julai 25, Tanzania huadhimisha kumbukizi ya mashujaa waliopigania uhuru wa taifa hili ambapo kwa mwaka 2024 maadhimisho haya yamefanyika jijini Dodoma kitaifa yakiongozwa na Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan. Theophilida Felician. Mkoa…

24 July 2024, 1:04 pm

CCM Missenyi yakemea utekaji wa watoto, yaitisha maombi

Kila mwaka wa uchaguzi kumekuwa na ongezeko la vitendo vya uhalifu ikiwemo mauaji ya makundi mbalimbali ya watu hali inayohusisishwa na ushirikina unaoaminika kufanywa na baadhi ya watu wenye nia ya kuwania nafasi mbalimbali za uongozi. Hali hii huamsha ari…

23 July 2024, 6:14 pm

EWURA CCC Kagera yapokea malalamiko 287, wananchi 9168 wafikiwa

Kutokana na changamoto zinazowakumba watumiaji wa huduma za nishati na maji nchini, Baraza la ushauri la watumiaji wa huduma hizo limekuwa na desturi ya kuwafikia na kuwashauri juu ya kutoa malalamiko yao pale wanapotendewa kinyume na matarajio Na Theophilida Felician.…

19 July 2024, 6:18 pm

MNEC Karim Amri aunga mkono ligi ya Bashungwa kwa mipira 50

Amesema hayo Julai 18, 2024 wakati akichangia mipira 20 kati ya 50 aliyoikusudia kwa ajili ya kuhakikisha ligi hiyo inafanikiwa kama ilivyopangwa na kuongeza kuwa Bashungwa ameanzisha ligi kwa wakati mwafaka ambapo kupitia kwa waratibu wa ligi na chama cha…

13 July 2024, 10:30 am

Changamoto za shule ya msingi Kitengule kutatuliwa

Na Eliud Henry Changamoto mbalimbali kwa shule za msingi na sekondari nchini zimekuwa kikwazo cha ufaulu na maendeleo ya watoto hasa linapokuja suala la miundombinu mibovu au chakavu na mabweni kwa wenye mahitaji maalum Shule ya msingi Kitengule inayohudumia watoto…

13 July 2024, 9:47 am

Miche milioni 3 ya kahawa kugawiwa bure Karagwe

Uchumi wa Karagwe unaendelea kukua kutokana na hamasa ya serikali kwa wananchi juu ya kuongeza nguvu ya upandaji wa miche bora ya kahawa na kuitunza. Na Shabani Ngarama Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Karagwe mkoani Kagera bw. Wallace Mashanda…

13 July 2024, 8:36 am

Wachungaji wapiga ramli, washirikina waonywa Kagera

Baadhi ya viongozi wa dini nchini ni miongoni mwa kundi la wahalifu wanaokamatwa katika maeneo mbalimbali kutokana na chunguzi zinazofanywa na jeshi la polisi. Miongoni mwa viongozi hao ni baadhi ya walimu wa madrasa wanaokamatwa wakituhumiwa kwa makosa ya ulawiti…

KARAGWE FM PROFILE

UTANGULIZI.
Radio Karagwe ni Radio ya kijamii iliyoanzishwa na shirika lisilokuwa la kiserikali lijulikanalo kama Karagwe Media Association (KAMEA).Ilianza kurusha matangazo yake Desemba 11.2007 kupitia masafa ya 91.4 MHz kwa ufadhili wa shirika la nchini Denmark (ULD80 Karagwe Venor) waliowezesha mafunzo kwa watumishi na upatikanaji wa vifaa.

DIRA.
Kuziba pengo la mawasiliano kwa wananchi wa Karagwe ambao kwa wakati huo hawakuwa na uwezo wa kusikiliza radio za Tanzania kutokana na jiongrafia ya eneo.

MAENEO REDIO INAKOSIKIKA
Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na ULD80 June mwaka 2012 Radio Karagwe ina zaidi ya wasikilizaji milioni 1.2.(KM 200 KUTOKA MAKAO MAKUU).Inasikika katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Kagera,katika wilaya za Karagwe, Kyerwa, Missenyi, Muleba na Bukoba Vijijini. Inasikika katika maeneo machache wilaya za Ngara, Biharamulo na Bukoba manispaa. Pia inasikika maeneo ya nchi jirani za Uganda, Burundi na Rwanda.

MAWASILIANO.
S.L.P 316,KARAGWE KAGERA TZ
E-mail : radiokaragwe@gmail.com
Phone: +255 754 677 708 / +255 689 471 171