Orkonerei FM

Lishe Bora Afya Bora.

23 September 2024, 8:02 pm

Orkonerei FM Radio kwa kushirikiana na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa(FAO) pamoja na Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania(TFNC) wameandaa kipindi cha Lishe Bora kwa ajili ya Jamii ya Kimaasai.

Ratiba ya Kipindi cha Lishe Bora Orkonerei FM Radio,

Na Baraka David Ole Maika.

Kipindi hicho cha Lishe Bora kina lengo la kuelimisha Jamii ya Kimaasai ulaji unaofaa kwa ajili ya kuimarisha afya ya miili yao kwa kutambua kuwa Afya ni Mtaji.

Kipindi cha Lishe Bora kimeandaliwa kwa mtindo wa maigizo kwa lugha ya kimaasai ili kufikisha ujumbe wa Elimu ya Lishe Bora kwa Jamii ya Kimaasai na Jamii zingine za kitanzania na kitarushwa kupitia Orkonerei FM Radio kila siku ya Jumanne saa 1:30 asubuhi na marudio siku hiyo saa 2:00 usiku na kitaanza kuruka kuanzia tarehe 24.09.2024.