Orkonerei FM

Wananchi Simanjiro wapatiwa vipimo bure

18 September 2024, 12:12 pm

Wananchi wakiendelea kupatiwa huduma na wataalam wa afya kutoka halimashauri ya wilay ya simanjiro (Picha na Joyce Elias)

Na Joyce Elius

Wataalam wa afya kutoka halimashauri ya wilaya ya simanjiro wameweza kutoa  huduma mbalimbali katika kata za Terrat Naberera  Emboreet  Kitwai na Orkesumet, huduma hizo ambazo zimegharamiwa na serikali kwa kushirikana na wadau wengine.

Akizugumza na Orkonerei fm Dr Godfrey Nyamkama amesema kuwa wananchi wameweza kujitokeza kwa wingi na wamepatiwa huduma kwa wakati.

Baadhi ya wananchi waliofika kupatiwa huduma wamesema kuwa huduma zinazotolewa ni nzuri na utaaratibu wa mapokezi hadi kuhudumiwa unafurahisha na zinawapunguzia gharama ya kwenda mbali kutafuta huduma.