Orkonerei FM
Kuna nafasi sawa ya kijinsia katika kumiliki ardhi?
8 May 2024, 3:10 pm
Na Joyce Elius.
Baadhi ya maeneo na jamii zimekua haziamini mwanamke katika kumilikisha ardhi na hii inatokana na mila na desturi za jamii husika.
Sera ya taifa ya ardhi ya mwaka 1995 inatambua kuwa wanawake na wanaume wana haki sawa yakupata, kumiliki, kutumia na kuuza ardhi, sera hii inalenga kuboresha hali ya wanawake katika maswala ya ardhi.
Fuwatana na mwanahabari wetu JOYCE ELIUS katika makala hii ambayo inaangazia namna familia ya Bwana Mosses wa kijiji cha Loswaki kata ya Terrat alivyomsaidia mkewe kumiliki Ardhi.