Karagwe FM
Karagwe FM
19 July 2024, 6:18 pm

Mbunge wa jimbo la Karagwe na waziri wa ujenzi Innocent Bashungwa ameendeleza utamaduni wake wa kutoa burudani kwa vijana jimboni humo kupitia ligi ya mpira wa miguu maarufu kama “Bashungwa Karagwe Cup”
Na Shabani Ngarama
Mjumbe wa halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi CCM Taifa kutoka mkoa wa Kagera Karim Amri amemshukuru mbunge wa jimbo la Karagwe na waziri wa ujenzi Innocent Bashungwa kwa kuanzisha ligi kwa vijana wilayani Karagwe kwa kuwa itasaidia kukuza vipaji na kuwawezesha vijana wengi kushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa baadaye mwaka huu na uchaguzi mkuu mwaka ujao
Amesema hayo Julai 18, 2024 wakati akichangia mipira 20 kati ya 50 aliyoikusudia kwa ajili ya kuhakikisha ligi hiyo inafanikiwa kama ilivyopangwa na kuongeza kuwa Bashungwa ameanzisha ligi kwa wakati mwafaka ambapo kupitia kwa waratibu wa ligi na chama cha mapinduzi kinapata nafasi ya kuhamasisha vijana kwenda kujiandikisha kwenye daftrai la kudumu la mpiga kura
