Karagwe FM

Wazee Missenyi waiomba serikali kuwalipia vipimo na matibabu

2 October 2025, 6:09 pm

Mwenyekiti wa wazee wilaya ya Missenyi mwalimu Renatus Leo. Picha na Respicius John

Imekuwa desturi kwa wazee kote nchini kulalamikia uduni wa huduma za afya kila inapofika Oktoba mosi na kuiomba serikali kuwapa unafuu wa maisha kwa kuwapatia penseheni na matibabu bila malipo.

Na Respicius John, Missenyi, Kagera

Wazee wilayani Missenyi mkoani Kagera wameiomba serikali kuboresha upatikanaji wa huduma za afya kwa wazee wote kwa kuhakikisha wanapata bure dawa na vipimo kuanzia ngazi ya zahanati wakati huo huo

Wakiongea katika maadhimisho ya siku ya wazee duniani yaliyofanyika kiwilaya katika kata ya Minziro wilayani Missenyi wameiomba serikali kuhakikisha wazee wote wanapata dawa na vipimo katika vituo vya kutolea huduma za afya

Baadhi ya wazee walioshiriki maadhimisho wilayani Missenyi

Baadhi ya wazee wakionesha mabango yenye ujumbe wa changamoto zinazowakabili. Picha na Respicius John

Kupitia risala ya wazee iliyosomwa na mwenyekiti wa wazee wilaya ya Missenyi mwalimu Renatus Leo wameeleza changamoto mbalimbali zinazowakabili na kuiomba serikali kuzishughulikia

Mwenyekiti wa wazee wilaya ya Missenyi mwalimu Renatus Leo
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Missenyi Juliana Lazaro. Picha na Respicius John

Kaimu mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Missenyi amesema kuwa serikali itaendelea kuwapa kipaumbele wazee wote kwenye suala la matibabu ikiwa ni pamoja na kuendelea kutoa vitambulisho vya matibabu bure suala ambalo liliungwa mkono na mgeni rasmi mkuu wa wilaya ya Missenyi Kanal mstaafu Hamis Mayamba Maiga

Kaimu DED Juliana Lazaro pamoja na DC Missenyi Kanal mstaafu Maiga
Mkuu wa wilaya ya Missenyi Kanal mstaafu Hamis Mayamba Maiga. Picha na Respicius John