Karagwe FM
Karagwe FM
14 July 2025, 8:13 pm

Wimbi la watu kujiua kwa madai ya kuchoshwa na ugumu wa maisha limeendelea kujitokeza katika maeneo mbalimbali nchini hal inayowasukuma viongozi wa dini kutoa mahubiri ya kuwatia moyo waumini wenye changamoto za maisha.
Na Theophilida Felician, Bukoba.
Imeelezwa kwamba jamii inapitia changamoto mbalimbali katika maisha hivyo ni vyema kila mmoja kwa nafasi yake kuchukua hatua na kumcha Mungu ili kuwatia nguvu na uvumilivu hatimaye kuzikabili badala ya kukata tamaa.
Ameyasema hayo mchungaji wa kanisa la EAGT MLIMA WA AHADI Clavery Venant lililopo mtaa wa Rwome Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera katika ibada ya jumapili iliyofanyika kanisani hapo.

Akitoa ujumbe wa maneno yenye kumtukuza mwenyazi Mungu amesema ili kuikabili mitihani ya ulimwengu haina budi kukaza maombi na kuyatenda yaliyo mema kwa Mungu na yeye atatenda na kuiponya mitihani hiyo.