TADEPA yaiasa jamii ya Kagera kuwekeza katika malezi
10 August 2024, 10:06 am
Suala la malezi na makuzi ya watoto limeonekana kutopewa kipaumbele na baadhi ya walezi na wazazi mkoani Kagera hali inayochochea udumavu wa kimwili na kiakili kwa watoto hasa waliokosa maziwa ya mama chini ya umri wa miaka miwili
Na Theophilida Felician.
Shirika la TADEPA ambalo ni shirika kinara katika utekelezaji wa mpango jumuishi wa malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto kuanzia umri wa miaka 0 hadi miaka 8 unaotekelezwa maeneo mbalimbali nchini, limeendelea kuihamashisha jamii mkoani Kagera kuwajibika kikamilifu katika majukumu ya malezi bora kwa watoto.
Akitoa kauli hiyo Abimeleck Richardi anayefanya kazi na shirika hilo kwenye banda lao viwanja vya maonyesho ya nane nane Kyakailabwa Manispaa ya Bukoba Agost 8, 2024 amesema kuwa wao kama shirika ambalo limekuwa na kipaumbele katika kutekeleza mpango huo bado jamii haijawa na mwamko madhubuti katika suala zima la kuwekeza kwa malezi.
Ameeleza kuwa wao kama shirika huwajibika vyema kwa kushiriki maeneo mbalimbali ya mikusanyiko ya watu ili kuhakisha ujumbe mahususi wa malezi bora unawafikia walio wengi.
Elimu ya programu ya malezi na makuzi bora ya mtoto imejumuisha makundi matano muhimu ya lishe, afya, ulinzi na usalama wa mtoto.
Amehitimisha akihimiza jamii na serikali kuthamini umuhimu wa kuwekeza kwa maslahi ya mtoto kwa umri mdogo.