Karagwe FM

CCM Missenyi yakemea utekaji wa watoto, yaitisha maombi

24 July 2024, 1:04 pm

Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Missenyi Alhaji Saidi Seluu akiwa na Askofu Samwel.Picha na Respicius John

Kila mwaka wa uchaguzi kumekuwa na ongezeko la vitendo vya uhalifu ikiwemo mauaji ya makundi mbalimbali ya watu hali inayohusisishwa na ushirikina unaoaminika kufanywa na baadhi ya watu wenye nia ya kuwania nafasi mbalimbali za uongozi. Hali hii huamsha ari ya serikali, taasisi za dini na wanaharakati kukemekea kwa nguvu zote vitendo hivi vinavyoashiria uvunjifu wa amani nchini

Na Respicius John

Viongozi wa dini wilayani Missenyi wameombwa kuendelea kuombea taifa wakati wa kipindi cha uchuguzi wa serikali za mitaa ili wapatikane viongozi bora na amani iendelee kutawala

Baadhi ya washiriki katika maombi yaliyoratibiwa na CCM (w) Missenyi. Picha na Respicius John

Kupitia maombi maalum ya viongozi wa dini wilaya ya Missenyi mkoani Kagera yaliyoandaliwa na chama cha mapinduzi CCM katibu wa chama hicho ngazi ya wilaya Bakari Mwacha amewaagiza viongozi wa dini kuliombea taifa na viongozi wake hasa wakati huu taifa linapoelekea katika uchaguzi wa serikali za mitaa na kwamba wilaya hiyo inaongoza kwa matendo ya hovyo likiwemo la utekaji wa watoto

Sauti ya katibu wa CCM (w) Missenyi Bakari Mwacha

Katika maombi yao baadhi ya viongozi wa dini waliopewa fursa waliekeza maombi yao kwa Mwenyezi Mungu kulinda maadili ya watanzania na kuwaepusha wananchi na uhalifu wa aina mbalimbali ikiwemo kuombea amani wakati wa uchaguzi

Baadhi ya viongozi wa dini wakifanya maombi

Akiongea kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya Missenyi kanal mstaafu Hamis Mayamba Maiga, katibu tawala wa wilaya ya Missenyi Bi Mwanaidi Mang’ulo amesema kuwa Tanzania inaamini katika maombi kwa kuwa hata katika wimbo wa taifa kuna maombi ikimaanisha kuwa kila jambo linategemea uwezo wa Mungu. Pia amewataka viongozi wa dini kufanya maombi kwa ajili ya taifa kila wakati jambo lililoungwa mkono na mwakilishi wa mwenyekiti wa kamati ya amani wilaya ya Missenyi Askofu Samwel Kasimbazi

Sauti ya katibu tawala wa wilaya ya Missenyi Bi Mwanaidi Mang’ulo
Baadhi ya viongozi wa dini wakishiriki maombi. Picha na Respicius John