‘Greening Karagwe Project’ kudhibiti nishati chafu Karagwe
8 May 2024, 9:37 pm
Kampeni kabambe kwa sasa hapa nchini ni ulinzi wa mazingira kwa kudhibiti ama kupunguza matumizi ya nishati chafu yaani kuni na mkaa. Afisa maliasili na mazingira wilaya ya Karagwe mkoa wa Kagera bw. Rajab Kassim akishirikiana na mashirika yasiyo ya kiserikali anaamua kuja na mradi wa kutengeneza Karagwe ya kijani kwa kubuni nishati mbadala ili kupunguza matumizi ya kuni na mkaa
Na Catus Tito
Halmashauri ya wilaya ya Karagwe mkoani Kagera kwa kushirikiana na mashirika yasiyo ya kiserikali imetambulisha mradi wa uhifadhi wa mazingira (Greening Karagwe Project) utakaogharimu zaidi ya shilingi bilioni sita.
Afisa Maliasili na mazingira wilaya ya Karagwe bw. Rajab Kassimu akitambulisha mradi huo wa uhifadhi wa mazingira (Greening Karagwe Project) kupitia mkutano wa baraza la madiwani wa halmshauri ya wilaya ya Karagwe wa robo ya tatu ya mwaka 2023/2024 Mei 7, 2024 amesema kuwa kwa kushirikiana na wadau halmashauri imekuja na mradi huo ili kutatua kero za uharibifu wa mazingira ikiwa ni pamoja na kutengeneza mkaa mbadala kufuatia tangazo la serikali la katazo la taasisi zote zenye watu zaidi ya mia moja kutotumia kuni na mkaa
Sauti ya afisa maliasili na mazingira bw. Rajab Kassim
Wakitoa mchango wao kuhusu mradi huo baadhi ya madiwani akiwemo diwani wa kata ya Nyakabanga Jastine Tinkaligayile Fidelis, Zidina Murshid wa kata ya Kituntu na Adrian Kobushoke wa kata ya Rugu wameipongeza halmashauri na wadau waliokubaliana kuanzisha mradi huo wakisema kuwa utachangia pakubwa katika ulinzi wa mazingira