Zenj FM

Skauti mashuleni, njia ya kukuza uzalendo kwa vijana

16 September 2025, 6:02 pm

Mkuu wa Wilaya ya Kati Unguja Rajab Ali Rajab akizungumza katika hafla ya kujitambulisha rasmi kwa walimu wakuu wa Wilaya hiyo, iliyofanyika katika ukumbi wa Afisi ya Walimu Kidimni.

Na wilaya ya Kati.

Mkuu wa wilaya ya kati Rajab Ali Rajab, amewataka walimu katika Wilaya ya hiyo kuanzisha vyama vya Skauti katika skuli zao ili kuwajenga wanafunzi kuwa wazalendo, wenye maadili na kuwasaidia kuwa raia wema wa baadaye.

Akizungumza katika hafla ya kujitambulisha rasmi kwa walimu wakuu wa Wilaya hiyo, iliyofanyika katika ukumbi wa Afisi ya Walimu Kidimni, Mkuu wa Wilaya Rajab, amesema vyama vya Skauti vina nafasi kubwa katika kuwalea wanafunzi kuwa viongozi bora wa baadaye.

Sauti ya Mkuu wa wilaya ya kati Rajab Ali Rajab.

Kwa upande wake, Mratibu wa Skauti Zanzibar, ambaye pia ni mjumbe wa Bodi ya Skauti Tanzania, Omar Abdallah Adam, amesema iwapo vyama hivyo vitaanzishwa mashuleni, ni lazima vizingatie misingi ya kielimu na si matakwa ya watu binafsi.

Sauti ya Mratibu wa Skauti Zanzibar.

Naye Mwalimu Mkuu wa Skuli ya Binguni Maandalizi na Msingi, Mwanamsa Maulid Ramadhan, akizungumza kwa niaba ya walimu wakuu wenzake, ameahidi kuwa watayatekeleza maelekezo yote yaliyotolewa, ikiwemo kuanzisha vikundi vya Skauti,ili kuhakikisha wanafikia lengo la serikali la kuwajenga vijana hao kimaadili.

Sauti ya Mwalimu Mkuu wa Skuli ya Binguni Maandalizi na Msingi, Mwanamsa Maulid.

Hafla hiyo imehudhuriwa na walimu wakuu 102 kutoka skuli za maandalizi, msingi na sekondari, wakiwemo kutoka skuli 16 za binafsi na 86 za serikali katika Wilaya ya Kati.